
Mwili wa askari huyo ukiwa eneo la tukio
Polisi
mkoani Dodoma wanamsaka mkazi wa Chang’ombe Juu, Tisi Malya kwa kumuua
askari polisi kwa kumcharanga mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wa
miezi minane aliyekuwa anataka kuuawa na mtu huyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amemtaja askari aliyeuawa jana majira ya saa 5:00 asubuhi kuwa ni Joseph Swai.
Akisimulia
mkasa huo kwa waandishi wa habari, Kamanda Misime alisema kuwa askari
huyo aliitikia mwito uliofika kwake wa kuwepo kwa dalili ya tendo la
jinai nyumbani kwa mkazi mmoja wa Chang’ombe Juu katika Manispaa ya
Dodoma.
Alisema
askari huyo alipigiwa simu na Mtendaji wa Mtaa wa Chang'ombe Juu,
akimjulisha kuwa amepokea taarifa ofisini kwake kutoka kwa Oliver
Baltazar(52) mkazi wa Chang'ombe Juu kuwa mtoto wake, Tisi Sirili
anaonekana anataka kumuua au ameshamuua mtoto wake wa miezi minane,
Valerian Tisi.SOMA ZAIDI>>>
0 comments:
Post a Comment