Posted by Williammalecela.com on Monday, February 16, 2015
 |
| "BOSSI TPA ASIMAMISHWA: Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta leo
amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari, Madeni
Kipande kwa kushindwa kuwajibika."... |
 |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -
Nimemsimamisha kazi kwa Muda Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Bandari Ndgu.Madeni Kipande leo hii trh 16 Februari 2015 ili kupisha
uchunguzi unaohusu tuhuma mbalimbali zinazomkabili.
Tuhuma hizo ni Pamoja na manung'uniko kuhusiana na ukiukwaji wa
taratibu za manunuzi .Hali hii inatokana na kutotabirika kwa taratibu
na kukosekana kwa uwazi , pamoja na taratibu hizo kuingiliwa na
mamlaka. Aidha
tuhuma nyingine ni mahusiano yasiyoridhisha kati ya Uongozi wa
Mamlaka ya Bandari na wadau wake muhimu na Mahusiano mabaya sehemu ya
kazi.
Kufuatia hali hii,nimeteua Tume ya kuchunguza suala hili na nimeipa
muda wa wiki mbili Kukamilisha kazi hii na kunipatia taarifa. Majina
ya Tume hiyo ni Kama ifuatayo :- 1.Jaji Mstaafu Agusta Buheshi-Mwenyekiti. 2.Ndgu.Ramadhan Mlingwa-Mjumbe 3.Eng.Samson Luhigo-Mjumbe 4.Ndgu.Happiness Senkoro-Mjumbe 5.Ndgu.Flavian Kinundo -Mjumbe 6.Ndgu.Deogratius Kasinda- Katibu Wakati
Ndgu.Kipande akiwa amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, kwa mujibu
wa Mamlaka niliyopewa na sheria ya Bandari Namba 17 ya Mwaka 2004
Kifungu Cha 34 Kifungu kidogo cha 2 ninamteua Meneja wa Bandari Dar
Bwana Awadh Massawe kukaimu nafasi hiyo kuanzia leo trh 16 Februari
2015. Samuel Sitta (Mb) Waziri wa Uchukuzi. 16 Februari 2015. |
0 comments:
Post a Comment