
SIKU
chache baada ya picha za mtoto mchanga kusambazwa katika mitandao ya
kijamii na kudai kuwa ni za mtoto wa mwimbaji wa nyimbo za Injili
nchini, Flora Mbasha kuwa amezaa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hatimaye wawili hao wamefunguka.
Hatua
hiyo imekuja miezi saba tangu wawili hao walipoingia katika mgogoro wa
ndoa yao hali iliyosababisha mume wa Flora, Emmanuel Mbasha kufikishwa
mahakamani kwa kosa la ubakaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana
ili kupata ukweli kuhusu taarifa za picha za mtoto huyo ambaye anadaiwa
kuwa amezaa na Flora, Mchungaji Gwajima, alisema taarifa hizo ni za
uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa Flora.
Mchungaji Gwajima
alikwenda mbali na kusema pamoja na uzushi huo unaosambazwa dhidi yake
kwa kuhusishwa katika uhusiano na Flora anamwachia Mungu kila kitu.
“Hahaha…
si unajua hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu…
wakati mwingine mimi huwa sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.
“Awali niliwaza kuwashitaki (alipoanza kuhusishwa kwamba ana uhusiano na Flora) wanaoeneza
uzushi huo lakini nikaona ‘It doesn’t hold water’ (haina mashiko), najua shutuma hizo zinatoka wapi,”alisema Mchungaji Gwajima.
Alipoulizwa
kuhusu mtu anayemshuku kueneza uvumi huo alisema:“Probably’ (nadhani)
atakuwa Emmanuel Mbasha mwenyewe. Tangu mwanzo alipotuhumiwa kumbaka
shemeji yake na kutoroka kwake akihofia kukamatwa na polisi, mkewe
alikuja kanisani kwetu na mimi nilimwagiza mwenyekiti wa kusaidia jamii
amsaidie,” alisema Gwajima na kuongeza:
“Sasa Mbasha alipotoka huko alikokimbilia na kusikia kuwa mkewe yuko hapa kanisani, ndipo alipoanza kueneza uzushi,” alisema.
Gwajima alisisitiza kuwa Flora hakufikia kwake kwa jambo lolote bali aliendelea kuishi katika nyumba aliyopanga.
Alipoulizwa
kwa nini hamshitaki Mbasha ili kulinda heshima yake, Gwajima alisema
ameshawaita ndugu zake akiwemo baba yake mzazi lakini nao wakaonekana
kutommudu Emmanuel.
“Nilishawaita wazazi wake, baba na mama
yake, ndugu zake kina Mbasha na tukazungumza. Lakini baba yake alisema
hata yeye amemshindwa. Yaani anawadharau hata ndugu zake,” alisema.
Akisimulia
jinsi alivyokutana na Emmanuel na Flora Mbasha, Mchungaji Gwajima
alisema awali walikuwa wakiimba kwenye mikutano aliyokuwa akihubiri.
“Hawa
hawakuwa washirika wetu, ila walikuwa wakija kuimba kwenye mikutano
yetu ya Injili. Walikuja Arusha, Moshi na Tanga, kwa hiyo tulikuwa
tukiwatumia sana. Baadaye ndiyo yakatokea hayo hadi Flora akakimbilia
kanisani kwetu,” alisema.
Hata hivyo Gwajima alisema hakujua kama Flora ni mjamzito wakati anakuja kuomba msaada kanisani kwake.
“Mimi
sikujua kama alikuwa mjamzito, hata taarifa kwamba amejifungua ndiyo
nazisikia kwako. Hapa nimetoka ‘airport’, sikuwepo Dar es Salaam,”
alisema na kuongeza:
“Sasa kama mtu una wasiwasi na mtoto si
ukapime DNA ili upate uhakika? Hii ni habari ya kutaka tu kulichafua
kanisa na huduma,”alisisitiza.Flora anena
Mwandishi alimtafuta Flora
kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hilo ambapo alisema “Siko tayari
kuzungumza lolote kuhusu Mbasha kwa sasa. Yeye anajeuri ya pesa ndo
maana anafanya haya yote lakini mimi ninasimama na Mungu wangu na
ninajua Mungu atanipigania,” alisema Flora.
Alipoulizwa
kuhusu hali ya mtoto wake mchanga, alisema “Mtoto hajambo, lakini mtoto
anayesambazwa kwenye mitandao siyo wangu, na hizo picha nyingine
nafikiri ni za kutengeneza tu,” alisema Flora.
Mbasha
Kutokana
na hali hiyo Mwandishi alimtafuta mume wa Flora, Emmanuel Mbasha, ili
kuzungumzia suala hilo, licha ya kupokea simu yake ya kiganjani,
aliishia kusema yuko njiani hivyo apigiwe baadaye.
Hata alipopigiwa baadaye, aliendelea kusema kuwa atafutwe baadaye na wala hakujibu ujumbe wa simu (sms).
Alipotafutwa
kwa njia ya ujumbe mfupi wa WhatsApp, ujumbe huo ulionekana kufika na
kusomwa na baada ya muda alituma ujumbe wa sauti uliokuwa na wimbo na
kuandika maneno mafupi yaliyosomeka ‘wimbo wangu mpya’.
Pamoja
na mambo mengine, wimbo huo unamaneno yasemajo “Haribu mipango ya
shetani, haribu…, Binadamu wengine mashetani mfano wa Cobra, wanawaza
mabaya, kuna siku watakufa kabisa,” ulisikika ujumbe wa wimbo huo
Sehemu
nyingine ya wimbo huo ulioimbwa kwa mwelekeo wa mipasho, inasema
“Wanakesha kwa waganga kuliloga, darubini ya bwana imewamulika, ukiwaona
utadhani ni wema,”
Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika tovuti
ya kituo cha televisheni ya East Africa (EATV), Agosti 27, mwaka jana
Flora alihojiwa na kituo hicho kupitia kipindi cha Kikaangoni Live,
kinachoendeshwa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema
ujauzito aliokuwa nao ni wa mumewe Mbasha na si Mchungaji Gwajima.
Flora
alisema kuwa hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mchungaji Gwajima
kwa kuwa ni mjomba wake na kwamba watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la
kumchafua na kumshushia hadhi.
“Hayo ni maneno tu ya watu mtaani
ila Mchungaji Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni ‘Uncle’ wangu
ninawezaje kuwa na uhusiano na uncle wangu..? ” alihoji Flora.
Kuhusu
kuachana na Mbasha, Flora alisema hakuachana naye kwa sababu ya Gwajima
na amedai kuwa bado anampenda, lakini anampenda Mungu zaidi.
“Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu,” alisema Flora.
0 comments:
Post a Comment