Posted by Williammalecela.com on Saturday, February 21, 2015
Mheshimiwa Lucy Mayenga Mkuu mpaya wa Wilaya ya Iramba na Mbunge wa Viti Maalum CCM.
Hizi picha 4 hapa juu ni za Mkuu mpya wa Wilaya ya Iramba Mheshimiwa Mbunge Lucy Mayenga, kwanza Wapinzani wamedanganya umma kuanzia jina la Mkuu huyo mpya wao wamemuita Lucy Mahemba wakati ukweli ni kwamba jina lake ni Lucy Mayenga, halafu Wapinzani wamedanganya umma kwamba ni mara yake ya kwanza kuteuliwa nafasi ya juu ya uongozi kwa sababu ni hawara wa Rais, wakati ukweli ni kwamba ni Mbunge wa muda mrefu wa Viti wa Maalum wa Vijana Shinyanga na pia amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui Tabora kwa Miaka 2 sasa na juzi Rais alichofanya ni kumhamishia tu Iramba na pia ukweli ni kwamba ni mke wa Mbunge wa Kibaha Vijijini Mh. Aboud. Wapinzani wamekuwa wakitumia kwa makusudi picha za Msanii maarufu wa bongo muvi Nice Chande hapa chini kumchafua Rais na Mkuu huyu mpya wa Wilaya bila sababu za msingi na in the process ni udhalilishaji wa kina mama kwamba hawawezi kushika nafasi kubwa za Taifa mpaka wawe mahawara wa Viongozi wa juu ni aibu sana. Rais JK amejitahidi sana kwenye uongozi wake kuwapandisha kina mama lakini kina mama wenyewe wamekuwa wakirudishana nyuma kwani waliotumika sana na Wapinzani kusambaza hizi picha ni kina dada wengi huko Social Media hasa Instagram lakini muongo mwisho wake siku zote huwa ni aibu kama hii hapa!! Wapinzani jifunzeni kwamba dola inashikwa kwa kushinda kura kwenye box sio kwa kuchafua kina mama wasio na makosa!! - Le Mutuz
0 comments:
Post a Comment