Ange Kagame hivi
karibuni amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii na kuzidi kujiongezea
umaarufu, hii sio tu kwasababu ni mtoto wa pili na wakike pekee kati ya
watoto wanne wa raisi Kagame bali muonekano wake wenye mvuto asilia umefanya
wengine kufikia hatua ya kumfananisha na Cleopatra.Ange alizaliwa mwaka
1989 na kwa mda mrefu amekuwa kwenye masomo nje ya nchi hivyo hajapata kufahamika
sana mpaka alipo msindikiza baba yake raisi Kagame kwenye hafla
ya jioni wakutanisha viongozi wa Afrika huko Marekani.
Picha zake zimepata
kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii na wengi wamesifia uzuri wake na kuweka picha
zake alizo piga kwenye matukio mbalimbali kwenye mitandao yao. ungana na ngastuka.com ili uweze
kumfahamu zaidi Ange kwa jicho la tatu, yani tuangalie maisha yake kwa ujumla
na mchango wake katika jamii kama kijana wa kiafrika.
Kwa mujibu wa IGIHE,
Ange ni msichana mwenye msimamo na kutegemea mazuri siku zote, mtu anaye tekwa
na hisia kali lakini pia ni msichana mtiifu na muaminifu, huku wenzake walio soma nae wakimsifia kuwa ana akili sana
darasani.
Ange hupendelea zaidi kula vyakula tofauti tofauti,
kutembelea migahawa mbalimbali hasa ile mipya na kusafiri. Kwenye michezo ana penda zaidi mpira wa kikapu na hushabikia Boston Celtics
timu inayo shiriki ligi ya kikapu ya NBA Marekani.
Kitendo cha hivi
majuzi cha kumsindikiza baba yake kwenye hafla ya jioni iliyofanyika ikulu ya Marekani kimehusishwa na jambo la kisiasa lakini yeye
mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Twitter ameshangazwa na hilo jambo na kukanusha skendo hiyo nakusema “huwa
mnakaribia lakini mnashindwa kugusa ukweli wa mambo”
Ukitazamia
ukurasa wake wa Twitter, Ange ameonekana kuwa ni msichana anaye pendelea zaidi
muziki michezo na burudani. Hata hivyo, amekuwa akishea nyimbo anazo zipenda zaidi kwa
marafiki na kipindi cha Kombe la dunia amekuwa akizipongeza timu za Afrika kwa
uwezo walio onesha, hii inaashiria kuwa sio mtu anaye zipa uzito habari za siasa labda kwa huko mbeleni.
Ange
amekuwa pia akishiriki kwenye matukio ya uchangiaji huko Kigali akisaidia
shughuli za maendelea,utoaji chanjo, elimu pamoja na kuwainua wanawake huku akifwata
nyayo za mama yake Jeanette Kagame ambaye
ni mwenyekiti wa mfuko wa Imbuto (Imbuto Foundation).
Kwa sasa Ange yupo mwaka wa mwisho wamasoma yake ya Chuo kikuu.



0 comments:
Post a Comment