Friday, February 6, 2015
Siku chache baada ya
kuzagaa picha zinazodai ni za mtoto wa muimbaji wa muziki wa injili,
Flora Mbasha na kuwepo tetesi kuwa huenda ni mtoto wa mchungaji Josephat
Gwajima, wawili hao wamelazimika kuzungumza.
Akizunguza na gazeti
la Mtanzania jana, kuhusu picha za mtoto mchanga zilizozagaa, Mchungaji
Gwajima, alisema taarifa hizo ni za uzushi na huenda zinasambazwa na
mume wa Flora.
“Hahaha… si unajua
hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu, wakati mwingine
mimi huwa sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.
“Awali niliwaza
kuwashitaki (alipoanza kuhusishwa kwamba ana uhusiano na Flora)
wanaoeneza uzushi huo lakini nikaona ‘It doesn’t hold water’ (haina
mashiko), najua shutuma hizo zinatoka wapi,” aliongeza Gwajima.
Hata hivyo Gwajima alisema hakujua kama Flora ni mjamzito wakati anaenda kuomba msaada kanisani kwake.
“Mimi sikujua kama
alikuwa mjamzito, hata taarifa kwamba amejifungua ndio nazisikia kwako.
Hapa nimetoka ‘airport’, sikuwepo Dar es Salaam,” alisema na kuongeza:
“Sasa kama mtu una
wasiwasi na mtoto si ukapime DNA ili upate uhakika? Hii ni habari ya
kutaka tu kulichafua kanisa na huduma,” alisisitiza.
Pia kwa upande wa
Flora alisema “Siko tayari kuzungumza lolote kuhusu Mbasha kwa sasa.
Yeye ana jeuri ya pesa ndo maana anafanya haya yote lakini mimi
ninasimama na Mungu wangu na ninajua Mungu atanipigania,” alisema Flora.
Alipoulizwa kuhusu
hali ya mtoto wake mchanga, alisema “Mtoto hajambo, lakini mtoto
anayesambazwa kwenye mitandao sio wangu, na hizo picha nyingine nafikiri
ni za kutengeneza tu,” alisema Flora.
Katika hatua nyingine
gazeti la Mtanzania lilimtafuta Emmanuel Mbasha, ili kuzungumzia suala
hilo, licha ya kupokea simu yake ya kiganjani, aliishia kusema yuko
njiani hivyo apigiwe baadaye.
Hata alipopigiwa baadaye, aliendelea kusema kuwa atafutwe baadaye na wala hakujibu ujumbe wa simu.

0 comments:
Post a Comment