Sio kila alichokichukia Mwl. Nyerere lazma ukichukie...... Kila mara huwa napenda kumtembelea Baba yangu na kuzungumza nae mambo mbalimbali. Lakini huwa hatuna msimamo wa pamoja wa jambo lolote lile, zamani tulikuwa tunabishana sana. Sikuhizi namsikiliza zaidi na kujengea hoja yake ninayoamini. Mara zote tunakubaliana kutokukubaliana. Mwl.Nyerere alikuwa na fikra zake alipoiongoza Tanzania, kwa wakati wake yalikuwa ndio maamuzi yake. Nationalization na free social service. Serikali ilifanya biashara. Mzee Mwinyi alikuwa na fikra zake, biashara ikapanuka na wananchi wakaanza kupata bidhaa zilizokuwa adimu. Mzee Mkapa amefanya yake, Privatization na tukaona sekta binafsi ikikuwa,kutoa ajira na KULIPA KODI. Dr.Kikwete ameendelea kuboresha
miundombinu, umeme vijijini(ambao ni mpango wake na Waziri yeyote akija utaendelea) na serikali yake imeongeza sekondari kwa 500% ambazo sasa tunazijengea maabara. Viongozi wote hawa waliongoza kwa muda wao na kufanya maamuzi kwa kipindi kile. Naamini kila mmoja ana fursa ya ku-challenge hasa ukizingatia mtazamaji mpira anaona zaidi ya mchezaji ("angepiga vile au hivi"). Sikuwahi kumwona Babu yake Baba na wala sijui habari zake, babu yangu yupo zaidi ya story sijajifunza mengi. Baba yangu yupo na tunaelewana sana ila mitazamo yetu mingi ni tofauti. Binafsi sifurahishwi sana na kauli "Kama Mwalimu angekuwepo" au "Kama Mwalimu angefufuka" naamini viongozi walioko wana cha kujifunza kwenye historia na yao ya kuamua kwa nyakati zao. Wanafunzi wa Sheria tunasoma majaji wakitofautiana mtazamo kwenye kesi moja yenye facts sawasawa. Sio kila aliyemchukia Mwalimu,lazma nawe umchukie kwa sababu zilezile......
0 comments:
Post a Comment