Saturday, February 28, 2015

Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba.

Stori: SHANI RAMADHANI wa GPL
Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kundi la Sanaa la Tanzania One Theatre (TOT), amekanusha habari zinazoendelea kuzagaa kwamba nyumba yake iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam imepigwa mnada na benki moja kutokana na madai ya kushindwa kulipa deni alilokuwa akidaiwa.
“Mheshimiwa anadaiwa na benki kama milioni 900, nyumba yake imepigwa mnada kwa sababu ameshindwa kulipa mkopo huo kwa muda aliopangiwa. Nasikia alichukua mkopo kwa ajili ya kuendeshea shule yake ya sekondari anayoimiliki jijini Dar matokeo yake ameshindwa kurejesha kiasi hicho kama mkataba unavyosema,” kilisema chanzo.



Baada ya kupata taarifa hizo, Uwazi Mizengwe ya Uchaguzi liliamua kumtafuta Mheshimiwa Komba ambapo baada ya juhudi za kukutana naye ana kwa ana kushindikana, mwandishi wetu alifanikiwa kuzungumza naye kwa njia ya simu.

“Hakuna kitu kama hicho, aliyetoa taarifa hizi ni muongo, kama mkopo nilichukua muda mrefu sana na mpaka sasa sijaona watu wakija nyumbani kwangu kwa madai kwamba wanataka kupiga mnada nyumba yangu siyo kweli,” alisema Kapteni Komba.

0 comments:

Post a Comment