![]() |
KATIKA hali ya kushangaza, bibi kizee anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka (70), asiyejulikana jina wala makazi yake,
ameanguka akiwa uchi wa mnyama nyumbani kwa Suzana Mwandu, mkazi wa Mtaa wa Mageuzi mkoani Shinyanga.Tukio hilo lilitokea juzi ambapo bibi huyo baada ya kuanguka alianza kutembelea makalio bila kuzungumza chochote jambo ambalo limedaiwa ni ushirikina.Akielezea tukio hilo jana, Mwandu alisema lilitokea nje ya nyumba ambapo alishangazwa kumkuta kikongwe huyo akiwa amelala huku akiwa uchi wa mnyama.Mwandu alisema baada ya kikongwe huyo kuanguka, alijivuta hadi kwenye jiko lake lililoko nje ya nyumba ambalo lipo wazina baada ya kuanza kumsemesha ndipo akazinduka na kuanza kuongea maneno yasiyoeleweka, hali ambayo ilimtia wasiwasi na kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Mtaa.“Nyumba yangu nimeizindika vilivyo, hivyo kikongwe huyu alipokuwa katika safari zake na kupita."

0 comments:
Post a Comment