![]() |
Bondia
Cheka: kama angeelimishwa umuhimu wa kuwa na Wakili, nina imani hadithi
ingekuwa tofauti, anaenda Jela, ndio wanatafuta wakili!!
Like ·
Israel Saria Leila Omary
mimi siyo mwanasheria, Ila kwa jinsi ninavyosoma habari za mwenendo wa
hukumu, ni kwamba aliambiwa ajitetee na Hakimu, naye akamwambia
Hakimu,hana cha kusema, je angekuwa na Wakili si angeshauriwa, sasa
utamlaumu nani?
Leila Omary Kwani kaka samahani unaposhambulia mtu hamnaga faini ni hukumu tu kaka angu ebu nielekeze sielewi
Shaibu De Ossu Israel
Saria Cheka ni mtu mkubwa na ni mtu muhinu ktk taifa hili ni kweli
alipaswa kuwa na mwanasheria wake ona sasa anaenda kuzika kipaji chake
jela!
Hassan Muhiddin Kosa
la kushambulia na kudhuru mwili (assault occasioning actual bodily
harm) halina faini na adhabu yake ni kifungo cha miaka mitano, kwa
mujibu wa sheria za Tanzania. Cheka anapaswa kumshukuru hakimu kwa kuwa
"lenient" na kumfunga miaka mitatu tu.
Kambi Abdallah Amestahili
kufungwa... Alikuwa na muda wa kutosha kutafuta wakili. Lakini pia
proffession yake haimruhusu kupiga/kupigana na watu wasio mabondia. Hilo
nalo halijui?
Israel Saria Leila Omary:
alichofanya Cheka ni( GBH) Grievous Bodily Harm) -Really serious harm"
alitakiwa tangu mwanzo apate ushauri toka kwa mwanasheria na atumie pesa
zake kutafuta unafuu, kwa hapa Uingereza hilo ni kosa kubwa sana,
lakini bado narudia kwanini uendekeze hasira. Namsikitikia kwa kutokuwa
na washauri wazuri, huku naamini hukumu inaendana na kosa! Pole
Mpale Mpoki Saria
nakubaliana na wewe kabisa, lakini kumbuka hasira ni human nature, kila
binadamu ameumbwa na hasira kumlaumu kwa kuwa na hasira ni kosa. Naomba
tulichukulie suala na Cheka kama suala la raia kadhaa ambao wanasimama
kizimbani bila kuwa na wakili. ...See More
Peter Shundi Mawazo yake yalivyomtuma ndivyo yalivyompoza, this is not a traffic case!
Hassan Muhiddin Ni
kweli Cheka hakupata ushauri mzuri. Inawezekana alitegemea umaarufu
wake ungemsaidia katika kesi hiyo. Hakujua kwamba sheria ikitumika
ipasavyo huwa haiangalii umaarufu wa mtu au nafasi yake katika jamii.
Mpale Mpoki Israel Saria
actually aliambiwa ajiteteee, akasema hana cha kusema, nasoma inaonesha
mashihidi wanne waliitwa upande wa mashitaka labda aliamua njia ya tatu
ya kujitetea yaani kukaa kimya ambayo inaipa room mahakama kuamua kesi
ya kwa inference. Kama u...See More
Israel Saria Mpale Mpoki-
Asante sana kwa ushauri, na kunielimisha, nilidhani unapokuwa na
mafanikio kama hayo ya Cheka, basi suala la kuwa na wakili ni moja kwa
moja! Na je alikuwa chini ya kampuni yoyote au alikuwa "solo"?
Jovent Johansen Anaweza
akakata rufaa tu na hamna namna nyingne nakubaliana nanyi hakuwa na
mshauri mzuri na hii ni tabia ya watu wengi maarufu na wenye kipato cha
kati, kitu kidogo tu utaskia nitakupoteza kijana unanijua mm ni
shida.Kwa hakika mahakama imempa adhabu stahiki.
Leila Omary Alipo
uko anajuta basi kama tatzo Ni ushauri akitoka kajifunza kitu bahati
mbaya ni kwamba nchi za wenzetu ukiwekwa ndani mtu maarufu,umaarufu
unazidi coz media zitakulipoti kila muda so ukitoka unakuwa maarufu
zaidi ya,,, lakini kwa nchi yetu unazidi kushuka thamani maana media
hazina huo muda media zenyewe mpaka uzipe kitu kidogo ndo zilipoti
habari zako (NCHI YA KITU KIDOGO)
Mbwana Mnose Israel Saria
hili ni funzo kubwa sana kwa wanamichezo wetu na hata sisi watu wa
kawaida,nadhani kilichomponza CHEKA ni kuishi kwa kujiona yupo juu ya
sheria (mfano chenge na kusababisha ajali iliyoua wale wasichana), na
pia kuishi kwa kudharau sheria z...See More
Mpale Mpoki unajua magazeti yote ya leo hakuna hata moja lililoandika kuhusu the way forward for him Israel Saria
sheria inamruhusu kuomba dhamana wakati anasubiri rufaa yake, na
wangejua hata jana hiyo hiyo kwa hakimu huyo huyo wangeweza omba dhamana
pending appeal. Tunaandika kishabiki zaidi kuliko constructive, kifungu
cha 368 cha sheria ya mwenendo wa kesi za jinai CPA
Honorary Edward Mallya Role
model wake ni Mike Iron Tyson... So anajaribu kumuiga kwa Kila kitu
kama Edo alivyosema.... Unless otherwise Inatuonyesha ni jinsi gani Ma
staa Wa hapa Nyumbani wapo nyuma. Ishu hiyo ingewezekana kabisa kuishia
nje ya Mahakama kwa kumlipa fidia mlalamikaji.
Honorary Edward Mallya Sasa Mpale Mpoki..
Tatizo ni kwamba hana washauri wazuri. Kama angekuwa nao asingalifikia
kifungo. Wasingekubali afungwe Kizembe Kiasi hiki.... Hivi mikataba yake
huwa anasainiwa au husaini tu bili kujua content?
Ally Bambo Umpa I
said the same!!...katka mitigation baada ya kua Convicted,aliulizwa
kwanin mahakama isimfunge,akajibu anaiachia mahakama yenyewe!! What a
mistake???
Mbwana Mnose Kinachoojadiliwa
hapa ni ukosefu wa maadili ambao cheka kama kioo cha jamii kaonyesha na
hili ni fundisho kubwa sana kwake..hakuna media hasa hawa waandishi wa
michezo kama waliweza kufuatilia mlolongo wa maisha yake ya kawaida
kabla ya kuwa maarufu unaweza kukuta alichofanya ndio mfumo wa maisha
yake.
Honorary Edward Mallya Na winning point za Appeal hutegemea makosa ya kiufundi na kisheria ktk mwenendo Wa kesi yenyewe. Mpale Mpoki....Do they Exist?
Honorary Edward Mallya Zipo nyingi sana Israel Saria
na Mororogo ndio inaahika nafasi ya 2 kwa Paralegals nyingi hapa
Bongo... Kwa kukosa Ushauri au Kudharau hakufika kupata Msaada Wa
Kisheria juu ya Kesi yake.. Je, Wao ndio wangemfuata ilhali yeye anao
uwezo Wa kuweka wakili??
Emmanuel Muga Hivi what happened? Alisema Hana cha kusema wakati wa mitigation au alivyotakiwa ajijitee baada ya prosecution ku rest?
Emmanuel Muga Cheka
hayuko kwenye category ya watu wanaoatahili msaada wa sheria bure,
alipaswa kumwajiri wakili, lakini kuwa na wakili haimaanishi kushinda
kesi wakati ushahidi umesimama vizuri unaoonyesha ulifanya kosa@saria
Honorary Edward Mallya That
is what we can say... Oscar Pistorious pamoja na kuua, Alipambana hadi
akafungwa miaka 3 badala ya 15 au Maisha. Hiyo ndiyo thamani ya kuwa
maarufu na kujielewa. Kesi ni kujenga hoja thabiti mbele ya Mahakama.
Israel Saria Emmanuel Muga
sasa nini sababu ya kuwa na wakili mzuri? Ni kwamba umefanya kosa, ila
unakuwa na wakili mzuri kutafuta mapungufu ya kisheria hatimaye
nionekane sina kosa, au nipate adhabu mbadala, ndiyo maana Watu wengi
mashuhuri huku Duniani wanatenda makosa, wanaishia kupata adhabu za
Kitoto..unanitisha bro! Lol
|
Tuesday, February 3, 2015
Posted by Williammalecela.com on Tuesday, February 03, 2015
1 comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




















Haswaa@wakili Muga. Anachokisema muga ndo sahihi. Wakili kazi yake ni kuraise doubts ambazo zitasaidia kupunguza gravity ya punishment na sio kutakatisha uhalifu.
ReplyDelete