MKALI
wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amepata shavu la kuwa balozi wa
kampeni ya kumsomesha mtoto wa kike ijulikanayo kama Morogoro Education
Development Organization (MEDO).
Mkali
wa sinema za Kibongo, Wastara Juma akisaini mkataba wa kuwa balozi wa
kampeni ya MEDO. Hafla fupi ya kusimikwa ubalozi huo na kusaini mkataba,
ilifanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Hoteli ya Tamal, Mwenge
jijini Dar ambapo baada ya kusaini, Wastara alianza kazi rasmi ya
kuhamasisha watu kuchangia elimu ya mtoto wa kike huku akiongozwa na
kauli mbiu ya kampeni hiyo isemayo ‘Sh. 500 yatosha kunipa elimu.’
Wastara Juma akipiga picha ya
pamoja na wadau wa kampeni hiyo. Wastara alishukuru kupewa nafasi hiyo
akieleza kuwa ni bahati kwake kwani wasanii wapo wengi.
“Ninawashukuru MEDO kwa kunipa
nafasi hii, niwaahidi kuwa nitaitendea haki kuhakikisha nahamasisha
uchangiaji wa fedha kwa ajili ya elimu ya watoto wa kike,” alisema
Wastara
0 comments:
Post a Comment