
Kutoka
kushoto: Waziri anayehusika na Shughuli za Baraza la Mawaziri Bi Stella
Ford Mugabo, Waziri Mkuu Anastase Murekezi,
Mkurugenzi mpya wa Ofisi ya
waziri Mkuu Bi Alphonsine Mirembe na Kimonyo James ambaye anakwenda
huko Kenya kuwa Balozi wa Rwanda (Picha/Kisambira T)Balozi Kimonyo alikuwa Mkurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, na nafasi yake hiyo imeingia chini ya udhibiti wa Bi Alphonsine Mirembe aliyekuwa Katibu wa Kudumu katika Wizara ihusikayo na shughuli za Baraza la Mawaziri. Katika kilele cha makabidhiano ya madaraka baina ya viongozi hao wawili, leo hii, Waziri Mkuu Anastase Murekezi amemmwagia sifa Balozi Kimonyo akisema anatumai atawakilisha vilivyo Rwanda huko Kenya, kwani ni mchakarikaji na ni mtu anayefanya kila kitu kwa wakati wake.
“Shukrani za dhati ziende kwa Rais Kagame ambaye ndiye alimteua kuwa kiongozi ofisini hapa, na ndiye amemteua kuwa balozi wa Rwanda nchini Kenya, hii ni kazi nzuri ambayo amepewa maana Kenya ni rafiki yetu sana, ni sehemu ambayo tuna biashara kedekede, na kama haitoshi ni sehemu ambayo tunaamini imetulia sana kiusalama,” ameongeza Murekezi.

Bi Alphonsine Mirembe na Balozi James Kimonyo wakati wanakabidhiana madaraka leo (Picha/Kisambira T)
Waziri Mkuu amesisitiza kuwa na imani kwamba Kimonyo anafaa kuwa balozi wa Rwanda nchini Kenya hasa ikizingatiwa jinsi alivyowakilisha vizuri Rwanda huko Washington kama balozi miaka ya nyuma. Licha ya kuwa balozi wa Rwanda nchini Marekani, James Kimonyo aliwahi pia kuwa balozi wa taifa hili nchini Afrika Kusini mwaka 2004.
Wakati akiwa huko Afrika kusini alikuwa ndiye anasimamia maslahi ya Rwanda katika mataifa lukuki mathalani Zambia, Msumbiji, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Swaziland na Lesotho.
Aidha, Balozi James Kimonyo alikuwa Gavana wa mkoa wa zamani wa Kibungo ambao hivi leo unapatikana katika Jimbo la Mashariki, kati ya mwaka 2002 na 2004. Baada ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi, Balozi Kimonyo alishikilia nyadhifa kibao katika serikali ya mpito, ikiwemo kuhusika na ujenzi na matengenezo ya miundo-mbinu mbalimbali iliyoathirika kipindi cha mauaji husika.
0 comments:
Post a Comment