Thursday, February 12, 2015

Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
KIMENUKA! Beautiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amemporomoshea matusi mazito shemeji wa Zarina Hassan ‘Zari’, King Lauwrance akidai amemuudhi sana kwa kitendo cha kuvujisha picha inayomuonesha akiponda raha nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ na mume wa Zari, Ivan Semwanga, Risasi Mchanganyiko linakupa mchapo kamili.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Wema na staa wa Bongo Fleva, Omari Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ walikwenda Sauz kurekodi video ya wimbo wa msanii huyo ambao jina lake bado halijafahamika
mara moja ndipo baadae picha ya Ivan, Wema na King Lawrence ilipovuja na kuzua gumzo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwa Sauz, baada ya Wema na Ommy kutua nchini humo na ‘project’ hiyo ya video, King Lawrance alidaiwa kuandaa mpango kabambe wa kuhakikisha kwa namna yoyote wanaonana na Wema kisha kupiga naye picha ambayo akiivujisha mtandaoni kila mtu ataamini wamefanya malipizi kwa zilipendwa wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye amemnyakua Zari, mke wa Ivan.

0 comments:

Post a Comment