Tukio
la mauaji limelotokea Mbeya, waliofariki ni mtoto mdogo mwenye umri wa
miaka mitano ambaye ameuawa na mjomba wake, wananchi wenye hasira
walimkamata mjomba huyo na kumuua pia.Watu hao waliokuja eneo hilo
walimkuta mjomba huyo akiwa amemuua mtoto huyo, wakaamua kumpiga mtoto
mjomba huyo ana yeye mpaka akafariki, baadaye wakamchoma na moto.
Baba wa kijana huyo ambaye ni mjomba wa mtoto huyo amesema kijana huyo alikuwa na matatizo ya kifafa kwa muda mrefu.
Baadae
wananchi hao walianza kuvamia nyumba hiyo iliyokuwa ikijengwa na kuanza
kuivunja na kuiba vitu mbalimbali kwa kuhusisha ujenzi wa nyumba
aliyouawa mtoto huyo na imani za kishirikina hadi Polisi walipofika na
kupiga bomu la machozi kutawanya watu hao.
Fundi
aliyekuwa eneo la tukio amesema mtoto huyo alifika eneo hilo wakawa
wanazungumza nae, ghafla akatokea mjomba wake akiwa na fimbo akaanza
kumuuliza maswali akakimbilia ndani kutafuta mlango wa kutokea,
akamkimbiza na kumkamata wakasikia kelele na kuingia ndani wakamkuta
kijana huyo akiwa na kisu mkononi na sururu akimchinja mtoto huyo,
wakaanza kupiga kelele kuomba msaada wananchi walipofika wakaanza
kumpiga na kisha kumchoma moto.
0 comments:
Post a Comment