ASKOFU
wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima jana alizimia na kisha
kukimbizwa hospitali wakati akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi Kanda
Maalumu ya Dar es Salaam.
Gwajima
ambaye alijisalimisha kituoni hapo saa 8:22 jana mchana akiitikia wito
wa polisi uliomtaka kufika kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi
ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama
Polycarp Kardinali Pengo.
Waandishi wa Mtanzania Jumamosi waliokuwa kituoni hapo wanaeleza kuwa walimuona Gwajima akitolewa kutoka katika chumba cha mahojiano akiwa amebebwa.Kwa mujibu wa waandishi hao Gwajima ambaye alikuwa amebebwa na maofisa wa polisi alipelekwa moja kwa moja kwenye gari aina ya Noah kwa ajili ya kumpeleka hospitali.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa 3:16 usiku lilikuja katika kipindi kisichozidi dakika saba tangu askofu huyo alipoonekana akiwa ameshikiliwa na wasaidizi wake kuelekea msalani huku yeye mwenyewe akiwa amejishika kichwa.

0 comments:
Post a Comment