Waziri wa Afya wa Zanzibar Rashid Seif Suleiman akikata utepe kuzindua mpango wa upimaji usikivu wa watoto wachanga katika hafla iliyofanyika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Mjini Zanzibar, wa kwanza (kushoto) mwakilishi wa WHO Zanzibar Dkt. Ghirmay Andemichael na (wakatikati) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Wafanyakazi wa Afya waliopatiwa mafunzo maalum ya kuwapima usikivu watoto wachanga wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) katika uzinduzi huo.
Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga. (kulia) Mkurugenzi wa Hospitali Kuu ya Mnazimmoja Dkt. Jamala Adam Taib na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Bi. Halima Maulid Salum.
Baadhi ya wageni walioalikwa katika uzinduzi wa kuwapima usikivu watoto wachanga wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Hospitali ya Mnazimmoja
0 comments:
Post a Comment