Wednesday, March 18, 2015

Kwa mujibu wa gazeti la Visa, limeripoti kuwa kuna fununu kuwa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja anadaiwa kurudiana na mzazi mwenzake P Funk Majani ambaye ni mtayarishaji nguli wa muziki wa Bongo Fleva. Hii ni kutokana ka bwana’ke amabe alimpora Wema Sepetu , CK kudaiwa kuishiwa mkwanja.


Licha ya kuwa Kajala bado yupo kwenye ndoa na mumewe anaesota gerezani, inadaiwa kwasasa anajipooza machungu na kushea mashuka ya hoteli na mzazi mwenzie P Funk. kwa mijibu wa gazeti hilo marafiki wa karibu wa Kajala waliliambia kuwa mara kadhaa Kajala amekuwa akitoka na P Funk kwa kificho, kwa kile kilichodaiwa anamwogopa mwandani wa sasa wa Majani.

Gazeti hilo liliendelea kueleza kuwa Kajala kwa sasa yupo dabo kwenye mahusiano na CK , bwana wa zamani wa Wema ambaye kwa sasa hali yake ya kiuchumi haina tofauti na Mr Nice.
Inadaiwa kuwa kinachosababisha ukaribu kati ya Kajala na P Funk ni mtoto wao Paula ambae kwasasa wanashirikiana vya kutosha kumlea.
Si Kajala wa P Funk aliyethibitisha habari hii

0 comments:

Post a Comment