Angelina Mziray Katibu Mkuu wa Women and Poverty alleviation in Tanzania , Akiwakaribisha wageni Mbalimbali waliofika katika Sherehe za Kuazimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo wao wameadhimisha mapema,Katika Ufunguzi Alisema kuwa Shirika lisilo ka Kiserikali la Waupata wakishirikiana na OXFAM wamesaidia Kijiji hicho katika kuleta maendeleo mbalimbali Tangu mwaka 2006 ikiwa ni pamoja na Kilimo cha mpunga, Matumizi Bora ya Ardhi.
Ambapo Pia aliwashukuru OXFAM kwa kuleta ufugaji bora wa kuku wa kienyeji, na ujenzi wa masoko mawili ya kisasa, Pia kusaidia wanawake kupata hati milili za Ardhi ambapo wanawake 186 watapata Hati hizo. Mwisho alishukuru taasisi zengine zisizo za Kiserikali ikiwemo Mviwata,Ungo,Tupawaki pamoja na Mwayodeo kwa jitihada zao za kusaidia wanawake na wanakijiji cha Gongoni katika maendeleo ya kijiji hicho.

Mmoja wa Mashuhuda Juliana Bi. Salum ambaye amepata haki Miliki ya Ardhi akielezea Jinsi gani ambavyo itamsaidia katika Maendeleo yake na jamii kwa ujumla.
Elizabeth Luoga ambaye pia amepata Hati Miliki ya Ardhi akielezea Furaha yake na Ushuhuda wake kwa kuwashukuru OXFAM kwa jitihada kubwa walizo zifanya na wanazo zifanya ili wanawake wapate umiliki wa Ardhi amewashauri wanawake kuwa umiliki wa Ardhi unawezekana.
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Gongoni, Kilichopo Kata ya Rudewa Tarafa ya Kimamba Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Bi. Grace Robertson Kanwakaita akitoa utambulisho kwa wageni mbalimbali ambao walifika katika Sherehe ya wanawake wakiwemo, Wakulima na wamama wafugaji walio katika eneo hilo,Opata,shirikisho la Ardhi,OXFAM, Mviwata,Ungo na wagani wengine waalikwa.
Profesa Majourin Mbilinyi Mwanamke mwanaharakati, Katika Sherehe hizo alisema kwamba wanawake wengi hawana kipato katika kupata umiliki wa ardhi, Ameipongeza Serikali ya kijiji ya Gongoni kwa kuwapatia Haki miliki ya ardhi wanawake alisema kuwa ipo haja ya kubadili mfumo wa umiliki wa ardhi kwa sababu ardhi ipo lakini wamiliki ni wenyefedha na iliyobaki kiasi ndio wanagombania wafugaji na wakulima wadogo wadogo na kusababisha Migogoro. Mwisho alisema kuwa wanawake wanahaki sawa ya kumiliki ardhi.
0 comments:
Post a Comment