
Muonekano wa kimini alichokuwa amevaa trafiki.
Mwandishi wetu Kimini alichovaa trafiki wa kike ambaye jina lake halikupatikana mara moja, kinadaiwa kuzua balaa huku wahuni wakimpigia miluzi.Tukio hilo lililojaza kadamnasi na kushuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri wiki iliyopita maeneo ya Mwenge jijini Dar, majira ya asubuhi.Bila kujua ‘amefotolewa’ trafiki huyo alikuwa amesimama pembeni akimtazama mwenzake wa kiume aliyekuwa akiongoza magari huku kimini chake cha sare ya kazi kikiwa kimepanda juu na kuonesha sehemu ya upaja wake wa haja.
“Jamani mbona majanga? Waone wahuni wanavyokitolea macho kimini cha trafiki na hapo amesimama. Akiinama kidogo tu mambo yote hadharani,” alisema mama aliyekuwa akiwashangaa raia walioacha kazi zao na kujadili kivazi hicho cha trafiki huyo.
0 comments:
Post a Comment