Monday, March 16, 2015

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akikagua barabara zote za Wilaya yake katika ziara yake ya ghafla kuona kama mvua kubwa ikinyesha hali halisi ya maisha itakuwaje kwa wananchi na makazi yao na hasa wananchi wanaoishi mabondeni. Katika kagua yake Mkuu alifanya hitimisho ya yafuatayo:- 1. Amewapa siku 7 Uongozi wa Hospitali ya TMJ kusafisha mitaro yao ya maji taka na kuyasafisha mazingira yao ama sivyo atawanyima kibali cha kufanyia kazi Wilaya hiyo. 2. Makonda amewaamuru Wananchi wote wanaoishi mabondeni kuhama mara moja kuepusha ajali kabla ya hatari ya Mvua ikija. 3. Amewaamuru wanaochimba mchanga karibu daraja la Mpiji kuacha mara moja kwani daraja hilo limeigharimu Serikali jumla ya Shillingi Billioni 4 sasa kwa kuchimba mchanga walikuwa wanapanua ukubwa wa mwanzo wa daraja ambayo itaishia kuliharibu daraja hilo. 4. Amewataka wananchi wote wa Kinondoni kujiaanda kuanza kuishi kwa usafi kwa kila mtu bila kusubiri kufanyiwa na Serikali.





0 comments:

Post a Comment