
Kutokana
na mvua kubwa zilizonyesha DAR na kuleta maafa ya mafuriko kwa baadhi
ya sehemu, nyumba ya kifahari ya msanii Diamond Platnumz ambayo ujenzi
wake haujakamilika nayo imekumbwa na madhara ya mvua baada ya ukuta wake
kuanguka.
Mtaalam wa majengo fundi Saidi amesema
tukio kama hilo linaweza kutokea kutokana ukuta kutowekwa zege la
kutosha chini, na juu inawezekana hapakufungwa mkanda.
Soudy Brown alimtafuta Diamond lakini hakuweza kumpata kwenye simu kwa muda mrefu, akamtafuta meneja wake ambaye ni Said Fella.
0 comments:
Post a Comment