Binti
wa miaka (14) aliyefahamika kwa jina la Latifa amejikuta akisutwa kwa
utapeli baada ya kunaswa na OFM akijifanya ni mtoto asiye na wazazi wala
ndugu wa kumsaidia.Binti huyo aliwasimulia waandishi wetu kuwa baba
yake alimtelekeza kwa majirani huko Dodoma maeneo ya Kibaigwa kwa kile
alichodai kuwa baba yake alikuwa na madeni yaliyosababisha mali zake
kupigwa mnada na yeye kusakwa ndiyo maana alikimbia.
Latifa
alisimulia kuwa kwa kuwa hakuwa na ndugu yeyote aliyekuwa akimfahamu
alilazimika kuishi maisha magumu ya kuhamahama akiwa peke yake ambapo
alidai alikimbilia kwa ndugu wa baba zake mkoani Lindi ambapo huko
alikutana na kasumba ya ukeketaji na kukimbilia jijini Dar.Akiwa Dar Latifa aliwasimulia waandishi wetu kuwa alikuwa akifanyishwa kazi nyingi kama hausigeli ndani ya nyumba moja maeneo ya Tegeta ambapo pamoja na hayo alikuwa akinyanyaswa sana.
Alizidi kudai kuwa aliamua kukimbilia Kijitonyama akiwa kama mzururaji ambapo alikutana na madada wanaojiuza ambao alidai kuwa walimchukua na kuishi naye mpaka alipokutana na waandishi wetu ambao aliwaomba msaada kwa madai hakuwa na chakula wala mahali pakulala .
AANZA KUSHTUKIWA
Hata hivyo, baada ya kupelekwa kwa mfadhili aliyeahidi kumpa malazi binti huyo, alimshangaza mwenyeji wake kwa kupigiwa simu mara kwa mara na watu ambao hakuwaweka wazi. Alipopekuliwa kwenye simu ndipo namba za watu waliogundulika kuwa ni ndugu zake walionekana na walipopigiwa walikiri kumfahamu Latifa kama ndugu yao na kuanika siri kwa nyakati tofauti kuwa kweli Latifa hana mama lakini tabia za utapeli zimemfanya afukuzwe kwa kila ndugu anayeishi naye.
“Yaani huyo mtoto hakuna mtu anayetaka kuishi naye mimi mwenyewe ameshaniliza na simtaki aje kwangu, nyie cha msingi mtoeni hapo nyumbani kwenu yasije yakawakuta,” alisema kaka yake aliyejitambulisha kwa jina la Saidi kauli iliyotiliwa mkazo na mama yake mdogo aliyejitambulisha kwa jina la Mwazani.
Hata hivyo, waandishi wetu waligundua kuwa msichana huyo kwa nyakati tofauti alienda nyumbani kwa wasanii wa filamu, Wema Sepetu, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael kwa nia ya kutaka wamasaidie lakini kashitukiwa na kutimuliwa.
“Nilienda kwa Wema nikagonga akatokea msichana akaniambia Wema hayupo nikawa narudia mara nyingi lakini mwishoni akanifokea. “Nikaenda kwa Lulu lakini mama yake alinifukuza na kwa Wolper niliambiwa alipokuwa akiishi alishahama,” alisema msichana huyo aliyedai yote aliyofanya ni kutokana na ugumu wa maisha hivyo asitiriwe.
0 comments:
Post a Comment