Monday, March 9, 2015

wa1Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo akimkaribisha Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari Zimbwini huko Kibiti, wilayani Rufiji, kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi vya WAMA katika mradi wa Mwanamke Mwezeshe tarehe 7.3.2015.wa2Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Ndugu Alife Omar Mtulia, Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya Mradi wa Mwanamke Mwezeshe wa Wilaya ya Rufiji wakati alipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Zimbwini zilikofanyika sherehe ya kutimiza mwaka kwa vikundi hivyo tarehe 7.3.2015.

wa3Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na mmoja wa Maafisa watendaji wa Mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika Wilaya ya Rufiji mara baada ya kuwasili huko Kibiti kuhudhuria sherehe za kutimiza mwaka za vikundi hivyo tarehe 7.3.2015.wa4Baadhi ya akina mama wa Vikundi vya Mwanamke Mwezeshe wa Wilaya ya Rufiji wakiimba nyimbo za mafanikio ya vikundi vyao wakati wa sherehe za kutimiza mwaka huko Kibiti, wilayani Rufiji tarehe 7.3.2015.wa5Wanachama wa Vikundi vya Mwanamke Mwezeshe wa Wilaya ya Rufiji wakiserebuka wakati wa sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi vyao zilizofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Zimbwini huko Kibiti wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani tarehe 7.3.2015.wa6Mamia ya wana vikundi vya WAMA katika Mradi wa Mwanamke Mwezeshe katika Wilaya ya Rufiji wanaonekana wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA wakati wa sherehe za kutimiza mwaka kwa vikundi hivyo. Sherehe hizo zilifanyika huko Kibiti na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Pwani.wa7

0 comments:

Post a Comment