"Naona kuna watu wanahangaika na kupoteza mda wao kwnda kujikusanya kwa mtu wakimuomba achukue fomu ya kugombea uongozi hapa nchini.

Nipende kuwambieni tu kuwa kwanza hizo wazifanyazo ni sarakasi zinazolenga kuishawishi taasisi yetu ya kisiasa imteue kwa lazima kwa mantiki kwamba ana ushawishi nje ya taasisi yetu kitu amabcho siyo kweli, pili ukiangalia kwa upande wa pili watu hao waendapo kwa mtu huyo hukuta viti, meza, vinywaji na chakula kimeandaliwa kwa ajili yao kitu amb
acho kinaonesha kuwa kuna mpango unafanywa na mtu huyo kuwahadaa Watanzania kuwa wamekuja wenyewe kumbe siyo.

Pili nipende kuwashauri wanavyuo wa Dodoma waache kujidhalilisha kwa kiasi hicho walichojidhalilisha leo na kuvivua nguo vyuo watokavyo hapa mjini Dodoma, mnaacha kusoma na kujikita kwenye utafiti mnatumiwa kwenda kuvuruga mchakato wa taasisi yetu.

Poleni sana kumbe kusoma sio kuelimika, bora hata mimi mtoto niliyeachwa yatima toka nikiwa na miaka 4 nikashindwa kupata elimu kwa sababu ya mazingira magumu ila ninazo akili za kuniongoza na kunionesha jema na baya."



Chanzo: WALL PAGE @ FACEBOOK LIVINGSTONE LUSINDE