Tuesday, March 31, 2015

Mkuu wa kitengo cha Branchless Banking and Business Development wa AccessBank

Tanzania, Mr. Andrea Ottina afurahishwa na mwenendo wa huduma za kubenki kupitia 

AccessBank WAKALA. Hayo yalibainika pale alipomtembelea mmoja wa mawakala  aliepo 
eneo la makumbusho na kufanya miamala mbalimbali mapema leo.


 Mkuu wa kitengo cha Branchless Banking Developing akipewa maelekezo na wakala jinsi ya kufanya miamala

Mr Ottina akifanya muamala baada ya kupata maelekezo
 Akijaza taarifa za muamala katika kitabu cha kumbukumbu cha AccessBank WAKALA

 Mr Ottina akifurahia huduma wakati wakala anaendelea kukamilisha muamala

 Mr Ottina akipokea pesa kutoka kwa Wakala
 Mr Ottina akiwa amekabidhiwa risiti baada ya muamala kukamilika

Aidha bwana Ottina, amewaasa wananchi kutembelea mawakala wa benki hiyo waliopo karibu 

nao ili waweze kufanya miamala balimbali ya kibenki kwa haraka na wepese zaidi. Baadhi ya 

huduma zinazotelewa kupitia AccessBank WAKALA ni kama vile, kuweka pesa, kutoa pesa, 

kufungua akaunti, kulipia bili za huduma mbalimbali kama vile LUKU, DSTV, DAWASCO na 

nyingine nyingi. 

Hivi Karibuni AccessBank Tanzania ilianzisha utoaji wa huduma zake za kibenki kupitia 

mawakala waliopo mtaani  Maarufu kama AccessBank WAKALA.  Mfumo huu umeiwezesha 

benki kuendelea kusogeza huduma zake karibu Zaidi na wateja na hivyo kuongeza urahisi wa 

upatikanaji wa huduma zake. 

kwa sasa huduma zinapatikana kwa Mawakala wafuatao; Skuvi 188 Mini Supermarket 

(Kijitonyama Shule - 0784 800573), Lacasumbai (Makumbusho – 0717 173084) na JK Internet 

Café’ (Mwenge Mpakani – 0713 477112). Mawakala wengine katika maeneo mbalimbali 

watatangazwa hivi karibuni. Wateja wanaombwa kutembelea mawakala hawa kujipatia huduma 

hata baada ya muda wa kazi wa matawi ya benki. kwa msaada zaidi mteja anaombwa kupiga ; 


0659 074000.

0 comments:

Post a Comment