Sunday, March 1, 2015



KAMPUNI ya Msama Promotions yenye maskani yake jijini  Dar es Salaam, imeendelea kuwa karibu kwa kuifikia jamii kwa karibu  baada ya kuwalipia ada  wanafunzi yatima  wa vituo vitano vya jijini Dar es Salaam waliokuwa wamesimamishwa masomo kwa sababu ya ukosefu wa ada.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Alex Msama japo ni utaratibu wa kampuni hiyo kusaidia makundi maalum katika jamii tangu mwaka 2000, hivi sasa wamejipanga kuongeza idadi ya vituo vitakavyopatiwa msaada wa ada.
Alisema kwa kuanzia wamekusudia  kuwalipia ada watoto yatima wa vituo 25 katika mikoa mbalimbali vikiwemo vitano vya jijini Dar es Salaam ambavyo ni Malaika Kids, Mwandaliwa, Honorata, Maunga Centre na Istiqama misaada ambayo wanajipanga kuifikisha mikoa ya Mbeya, Morogoro, Iringa, Ruvuma, Dodoma, Shinyanga na Tabora.
Msama alisema wamefanya hivyo kwa kutambua kuwa hilo ni moja ya malengo ya msingi ya tamasha hilo katika kipindi hiki cha maandalizi ya Tamasha la Pasaka ambalo mwaka huu linatimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake.
Aliongeza kuwa tangu kuasisiwa kwa tamasha hilo Kamati imetumia kiasi cha shilingi milioni 17 zimetumika kusomesha watoto yatima huku misaada kwa ajili ya wajane imefikia milioni 76 ambako pia wamejipanga kutoa baiskeli 100 kwa walemavu.

0 comments:

Post a Comment