Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa wa Airtel Bwana David Wankuru
akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye ni Mvuvi
na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka mshindi
wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa
Airtel Bi Jane Matinde
Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana
Kijiji Gweso akifungua gari mara baada ya kukabidhiwa gari na Airtel
mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi wa wilaya
ya Sengerema Mwanza. akishuhudia ni Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa
wa Airtel David Wankuru
Mshindi wa gari kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi Bwana
Kijiji Gweso akiwa ndani ya gari yake mara baada ya kukabidhiwa gari
na Airtel mara baada ya kuibuka mshindi, Bwana Gweso ni Mvuvi na mkazi
wa wilaya ya Sengerema Mwanza.
Kaimu Katibu wa Wilaya ya Sengerema Bwana Aaron L Laizer ( wa pili
kushoto0 akimkabithi gari aina ya Toyota IST bwana Kijiji Gweso ambaye
ni Mvuvi na mkazi wa wilaya ya Sengerema Mwanza mara baada ya kuibuka
mshindi wa promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi akishuhudia ni Afisa
Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde na Kaimu Meneja Mauzo Kanda ya Ziwa
wa Airtel Bwana David Wankuru
Mvuvi katika kisiwa cha Yozu wilaya ya Sengerema Aibuka na Toyota IST
Mkazi wa wilaya ya sengerma na mvuvi katika kisiwa cha Yozu bwana
Kijiji Gweso Jana amekabithiwa gari aina ya Toyota IST na kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel mara baada ya kuibuka mshindi wa promosheni
ya Airtel yatosha zaidi
Akiongea wakati wa halfa ya kukabithiwa gari lake Bwana kijiji Gweso
alisema” nilipopigiwa simu na Airtel nilipuuzia sikuamini kabisa kama
nimeshinda gari mpaka ndugu zangu waliponipigia na kunihakikishia kuwa
mimi nimetangazwa mshindi ndipo nilipoenda ofisi za Airtel na kukuta
kweli nimejishindia. Mimi ni mvuvi na mke na watoto wawili na
nilinunua kifurushi cha Airtel yatosha cha mia tano tu na furahi sana
kushinda gari hili kupitia promosheni hii”
“Sijawahi kumiliki gari hivyo usafiri huu utanisaidia katika shughuli
zangu za uvuvi, za kifamilia na kiuchumi kwa ujumla, nachukua fulsa
hii kuwaambia watanzania wenzangu waamini kuwa Airtel inatoa magari na
kwamba wao pia wanaweza kuwaibuka washindi. Nawashukuru sana Airtel
kwa kuboresha maisha yangu na yawatanzania wengine walioshinda kama
mimi”aliongeza Gweso
Akiongea wakati wa kukabithi gari kaimu katibu wa wilaya ya sengerema
bwana Aaron L Laizer alisema” nampongeza sana bwana Kijiji Gweso kwa
kuibuka mshindi, ushindi huu umetuthihirishia wakazi wa sengerema kuwa
promosheni hii ya ya ukweli na zawadi zinatolewa. Tunawashukuru sana
Airtel kwa kutoa huduma bora za mawasiliano nchini ambazo
zimerahisisha shughuli za kiuchumi, kijamii na kiusalama lakini pia
kuanzisha promosheni inayowazawadia wateja wake, na kwa wananchi wa
sengerema na wa mwanza kwa jumla hii nifulsa kwetu tuendelee kutumia
huduma za Airtel na kupata nafasi ya kushinda”
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa kanda ya Airtel Bwana David Wankuru
alisema “ promosheni hii bado inaendelea mpaka sasa ni washindi 24
tumeshapatikana , magari bado yapo hivyo natoa wito kwa wakazi wa
kanda yangu na watanzania kwa ujumla kuweza kushiriki. Tunafurahi kuwa
na washindi wane mpaka sasa kutoka katika kanda ya ziwa washindi hawa
ni pamoja na Bi Ester Mathias Mashauri muuguzi bugando, Bi kajala
kokutima said mkulima na mkazi wa bukoba, Seleman Daudi Onesmo mkazi
wa nyakato Mwanza na leo tunamkabithi gari bwana Kijiji Gweso mkazi wa
Sengerema’.
Wankuru aliongeza kwa kusema “kujishindia unatakiwa kujinga na
kifurushi chochote cha Airtel yatosha cha siku, wiki au mwenzi kwa
kupiga *149*99# au kununua vocha ya Airtel yatosha au kwa kununua
kupiita huduma ya Airtel Money, baada ya kununua kifurushi chako namba
yako moja kwa moja itaingizwa kwenye droo na kupata nafasi ya
kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku”.
Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi ilizinduliwa na kampuni simu za
mkononi ya Airtel Mwanzoni mwa mwenzi wa Februari, watanzania wengi
kutoka katika mikoa mbalimbali wameweza kujishindia magari na kubadili
maisha ya kupitia promosheni hii. Magari 24 yameshapata washindi toka
promosheni hii ianze hadi sasa.




0 comments:
Post a Comment