Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Cecilia Mosha (26) aliyejirusha kutoka
ghorofa ya tatu hadi chini kutokana na hofu ya moto uliotokea katika
Hosteli ya Mabibo, amevunjika mfupa wa bega.
Mwanafunzi
huyo alijirusha kupitia dirishani juzi katika harakati za kujiokoa na
moto baada ya jengo la wasichana, Block B kushika moto. "
Nilisikia
kelele za moto nikiwa chumbani na nipotoka nje nikakuta moshi umetanda
kila kona, baada ya kuona hivyo niliona ni vema nijiokoe kwa kujirusha
kutoka ghorofa ya tatu ya bweni hilo hadi chini kupitia dirishani,”
amesema Cecilia Mosha
0 comments:
Post a Comment