HII ni habari ya kutisha! Takriban miaka mitatu imekatika tangu kifo cha
aliyekuwa staa wa Bongo Movies, Steven Kanumba huku watu wawili
wakifariki dunia kwa nyakati tofauti lakini nyuma ya pazia ya vifo vyao,
mzimu wa Kanumba unatajwa kuhusika kutokana na watu hao kutaka kuishi
mahali pa marehemu huyo, endelea kusoma Risasi Jumamosi.SOMA TUKIO HILI LA KUSHANGAZA
Itakumbukwa
kwamba, baada ya kifo cha Kanumba, mama yake mzazi, Flora Mtegoa ndiye
aliyeshika jukumu la kusimamia mali za marehemu mtoto wake (alikuwa na
haki).
Miongoni
mwa mali hizo ukiachilia mbali, magari, vifaa vya kurekodia filamu,
viwanja na filamu zilizokuwa hazijalipwa, mama Kanumba aliimiliki ofisi
ya Kanumba iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Kanumba The Great Film
iliyokuwa Sinza.Hata hivyo, hivi mapema Februari, mwaka huu, mama
Kanumba alitoa vitu kwenye ofisi hiyo kwa madai ya kushindwa kulipa
pango, hivyo ofisi ikawa wazi.
KILICHOTOKEA SASA
Habari
ambazo gazeti hili ilizipata zilidai kwamba, mpangaji mwingine
aliikodisha ofisi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini hivi karibuni
mtu huyo amefariki dunia.Msikilize shuhuda: “Kuna jamaa alipanga kwenye
ofisi iliyokuwa ya Kanumba mara tu baada ya mama Kanumba kuondoka vitu
kwa kushindwa kulipia mkataba mpya.
“Huyo
jamaa alikuwa anahusika na masuala ya ujenzi. Jamaa alilipia kodi ya
mwaka mmoja, akawalipa watu wamfanyie usafi yeye akaenda ‘saiti’ kwenye
mambo yake ya ujenzi. Inadaiwa akiwa kule, kuna ‘kijiko’ kilichokuwa
kinachimba kiwanja, bahati mbaya kikarudi nyuma na kumgonga, akaanguka
na kufariki dunia.”
JE, NI MZIMU WA KANUMBA?
Kifo
cha mtu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja,
kinaunganishwa na tukio lilitokea mwaka juzi baada ya kifo cha Kanumba
kilichotokea Aprili 7, mwaka 2012.Mara baada ya Kanumba kufariki dunia
ghafla, mwanamke mmoja alikwenda kupanga nyumba ile aliyokuwa akiishi
marehemu iliyopo Sinza, Dar, naye alifariki dunia ghafla.
MAJIRANI WALIZUNGUMZA
Wakati
wa tukio hilo, wanahabari wetu walifika nyumbani kwa mwigizaji huyo
ambapo walizungumza na majirani wakaelezea juu ya uwepo wa tukio
hilo.Walisema japo hawaamini juu ya imani za masuala ya mzimu wa
marehemu lakini kitendo cha mwanamke huyo kufariki dunia muda mfupi
baada ya Kanumba kufa kiliwafanya washtuke na kuamini kwamba huenda ni
mzimu wa Kanumba ndiyo ulichukua roho ya mpangaji huyo.
WENGINE WALIAMINI HIVI
Hata
hivyo, baadhi ya watu wengine pia walisema yao wakidai kwamba,
wanaamini kifo cha mwanamke huyo ni cha kawaida kama ilivyo kwa vifo
vingine.“Kama siku za Kanumba zilivyokuwa zimewadia na huyo mpangaji pia
siku zake zilikuwa zimefika ndiyo maana amefariki dunia,” alisema mmoja
wa majirani.
ALIVYOSEMA MZEE ALIYEKULA CHUMVI NYINGI
Mzee
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Mohamed Sumali (76), mkazi wa
Mabibo-Relini, Dar akizungumza na gazeti hili kuhusu mazingira ya vifo
hivyo, alisema:“Ipo mizimu ya hivyo. Mtu akifa, wa kwanza kuhamia kwenye
nyumba aliyokuwa akiishi marehemu naye anakufa. Lakini si kwamba nyumba
ndiyo ina mizimu. Kama hivyo vifo vimetokea kweli basi na mzimu wa
Kanumba umeshaondoka.”
MAMA KANUMBA AZUNGUMZA
Baada
ya kuzipata habari hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya mama Kanumba
kutaka kujua kama anajua lolote juu ya marehemu mtoto wake kuacha mzimu
ambao unahusishwa na vifo hivyo ambapo alikiri kusikia taarifa za kifo
cha jamaa aliyepanga kwenye ofisi za Kanumba lakini akasema hata yeye
hajui sababu za kifo chake.
“Hata
mimi nimesikia, lakini sielewi chochote kuhusiana na mtu huyo kufariki
dunia. Imenishtua kwa kweli maana si unakumbuka hata kule alikopanga
(Kanumba) mwanzoni nako aliyepanga ile nyumba naye alifariki? Sijui hata
ni kwa nini?” alihoji mama Kanumba kwa sauti iliyoashiria kushangaa
sana.
0 comments:
Post a Comment