Posted by Williammalecela.com on Saturday, March 07, 2015
Akishiriki na katibu mkuu wa CCM Taifa na viongozi wengione wa chama katika ujenzi wa mradi wa maji eneo la Mnarani, mjini Unguja hivi karibuni.
Baadhi ya vitendekazi alivyovitoa kwa wakazi, vikundi na viongozi wa chama jimboni kwake, Kikwajuni.
…………………………………………………………………..
Visiwa vya Zanzibar vinakabiliwa na changamoto nyingi lakini kubwa ni ukosefu wa ajira kwa vijana, uraibu wa dawa za kulevya, mzunguko mdogo wa fedha na ongezeko la idadi ya watu ambalo halilingani na raslimali zilizopo.
Wenyeji wanafanya jitihada tofauti kulabili hali hiyo ikiwa ni pamoja na kubuni miradi ya uzalishajimali, vikundi vya elimu kwa walaibu wa dawa za ulevya na pia vya uzalishajimali wakiamini kuwa zikiwepo ajira za kutosha matukio yasiyofaa yatapungua.
Hata hivyo kama ilivyo katika maeneo mengine, wakazi hao wana viongozi wao wakiwemo wa kuteuliwa na kuchaguliwa na wananchi ambao ni masheha, wawakilishi na wabunge achilia mbali mawaziri na watendaji wengine.
Kwa kushirikiana na watendaji hao wananchi wanajitahidi kukabili changamoto tofauti zinazowakabili lakini katika hali isiyo ya kawaida, kuna makundi na wanasiasa visiwani humo ambao wamekuwa wakipeleka misaada kwa wapiga kura wao ambao hata hivyo haijaleta matokeo chanya.
Vipaumbele vya wakazi
Mbunge wa Kikwajuni (CCM), Hamadi Yussuf Masauni anasema hali hiyo inatokana na sababu nyingi lakini kubwa ni ukweli kuwa misaada hiyo sio kipaumbele cha wananchi hao ambao wakati mwingine hupokea na kujadili baadae cha ufanya na msaada huo.
Masauni anasema wananahci katika maeneo yao wana vipaumbele vyao hivyo ni vema wanasiasa kuzungumza nao na kujua mahitaji yao kabla ya kukusanya nguvu za kutanzua kero hizo na uzoefu huo ameupata baada ya kuutumia katika kipindi cha miaka mitano iliyopita jimboni mwake.
Anasema kazi ya kwanza ilikuwa kutembelea vikundi, ofisi za chama cghake, maskani na maeneo menione kwa ajili ya kujua shughuli zinazofanyika na changamoto zilizopo, ziara ambayo ilipanua wigo wake wa ufahamu na kuweza kutambua vipaumbele vya wakazi.
Anabainisha kuwa alikutana na vikundi vya uzalishajimali ambavyo vilikuwa na changamoto ya mitaji, vitendeakazi na mahitaji mengine ambavyo ni pamoja na Benki ya Kikwajuni Saccos, timu za soka, maskani za CCM, shule za awali, jumuia za wanawake, wenye ulemavu, wazazi, vikundi vya sanaa na utamaduni.
Taasisi zingine ni pamoja na Tanzania Youth Icon (Tayi) ambacho kinawajumuisha vijana katika shughuli za Polisi Jamii, uapishi wa vyakula vya aina mbalimbali, dawa, wanyanyua uzito, wacheza muziki wa dansi, watengenezaji wa mapambo na maua na huduma zingine.
“Wote tulikaa pamoja na kuzungumza na walinieleza mahitaji yao na karibuni hapa nimewaita mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana na kuwapatia walichohitaji” anasema na kuongeza kuwa mahitaji yalikuwa makubwa lakini hata hivyo amefanikisha.
Anabainisha kuwa ametumia kiasi cha sh.150 milioni kwa ajili ya kuwapatia mahitaji wakazi wa jimbo hilo ikiwa ni pamoja na gari aina ya Suzuki kwa benki ya Kikwajuni Saccos na msaada wenye thamani ya zaidi ya sh2 milioni kwa kikundi cha Tayi ambacho kinaundwa na vijana zaidi ya 500.
0 comments:
Post a Comment