Sunday, March 22, 2015

111Na Anitha Jonas- MAELEZO,Dodoma.
Serikali imepinga Suala la kuanzishwa kwa Mwenge utakao kuwa unakimbizwa kwa kila Mkoa kwa dhana ya kujaribu kupunguza gharama za Mbio za Mwenge nchini,hayo aliyasema Naibu Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia alipokuwa akijibu swali Bungeni Mjini Dodoma.
Mheshimiwa Nkamia alisema kuwa kuanzishwaji kwa Mwenge kwa kila Mkoa kutaondoa dhana halisi ya kuwepo kwa Mwenge nchini kwani falsafa ya Mwenge ni Mshikamano kwa Taifa,Umoja kwa Taifa,Amani kwa Taifa pamoja na Maendeleo kwa Taifa.

“Suala la kuwepo na Mwenge mmoja Kitaifa ni kitu sahihi kabisa na hata tukiangalia nchi za wenzetu mfano Jumuiya ya Madola wanakifimbo cha malkia ambacho huzungushwa katika nchi zote za Jumuiya ya Madola,pia upo Mwenge wa Olimpiki ambao huzungushwa dunia nzima hivyo si busara kwa nchi yetu kuanzisha utaratibu wa Mwenge kwa kila Mikoa”,alisema Nkamia.
Hoja hiyo ya kupunguza gharama za mwenge pamoja na suala la kuanzishwa kwa Mwenge katika mikoa ni swali lilihojiwa na Mhe.Meshark Opulukwa Mbunge wa Meatu katika kipindi cha maswali na majibu na huku akiishauri serikali kutengeneza Mwenge huo hata kwa mabati chakavu kupunguza gharama.

0 comments:

Post a Comment