Msanii
wa muziki, Nuh Mziwanda, ametoa kali ya mwaka kwa kudai kwamba kitendo
cha kupigwa mara kwa mara na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,
kinampa furaha na ufahamu wa namna anavyopendwa.Akizungumza na gazeti la
Mtanzania, Nuh alisema kupigwa kwake ndo ishara ya mapenzi kutoka kwa
mpenzi wake huyo.
“Kwanza
kupigwa raha, mpenzi wako asipokupiga hakuonei wivu, mimi nafurahi sana
na namtaka anipige tu! kila siku akijisikia, ananidhihirishia kuwa
ananipenda,” alisema.
Nuh
alisema mengi yamesemwa kutokana na kupigwa kwake mara kwa mara, huku
akidai kwamba hilo halina tatizo kwake, kwa kuwa halitaharibu mapenzi
yao wanayoamini yatafika mbali.
“Sisi tunawezana na Mungu atusaidie tufikie katika hatua ya ndoa tuliyojiwekea,’’ alimaliza.

0 comments:
Post a Comment