Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Msanii nguli wa muziki wa kizazi kipya na nyota wa Wimbo wa Nitampata
wapi aliyewahi kuwa mchumba wa Wema Sepetu, Nasibu Abdul ‘Diamond’
amenusurika kukatwa mguu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar
es Salaam
kufuatia ugonjwa wa Foot Corn (maarufu kwa jina la kisahani)
kumtesa kwa kipindi kirefu. Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Diamond ambaye kwa sasa anaminya
kimalavidavi na mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’, alianza kusumbuliwa na
ugonjwa huo takribani siku 730 zilizopita (miaka miwili), huku mwenyewe
akipuuzia matibabu yake na kuelekeza nguvu kwenye shoo za ndani na nje
ya nchi.
“Mara kwa mara alikuwa akilalamikia maumivu makali ya mguu
lakini kwa kuwa yalikuwa yakija na kupotea, alikuwa akipuuzia kwenda
hospitali mpaka juzi (Ijumaa) alipoamua kwenda TMJ,” kilisema chanzo
chetu kwa masharti ya kutotajwa jina.

0 comments:
Post a Comment