Wednesday, March 4, 2015

Afisa uandikishaji katika Daftari la kudumu la wapiga kura, Alen Simon (kulia) akichukua taarifa muhimu za wakazi wa Mangula Makambako walijitokeza kujiandikisha katika kituo cha kata ya Mjimwema. Picha na Shaban Lupimo. 
Na Geofrey Nyang’oro,
Tume ilianza kazi ya kuandikishwa wapiga kura kwenye kata tisa za Kitisi, Kivavi, Lyamukena, Maguvani,Majengo, Makambako, Mjimwema, Mlowa na Mwembetogwa katika mji huo wenye kata 12 na leo inahitimisha katika kata hizo na kuanza katika tatu zilizobaki.
Makambako. Wakazi wa Mji wa Makambako, mkoani Njombe wamevuka lengo lililowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) la kuandiksha watu 32,370 katika Daftari la kudumu la Mpiga Kura, ambalo unatumika mfumo mpya kuandikisha wa Biometrick Voters Regstration (BVR) na kufikia watu 39,579, huku kazi hiyo ikitarajiwa kuhitimishwa leo katika kata tisa za mji huo.Tume ilianza kazi ya kuandikishwa wapiga kura kwenye kata tisa za Kitisi, Kivavi, Lyamukena, Maguvani,Majengo, Makambako, Mjimwema, Mlowa na Mwembetogwa katika mji huo wenye kata 12 na leo inahitimisha katika kata hizo na kuanza katika tatu zilizobaki.
Idadi hiyo ya wapiga kura imevuka lengo, huku kazi hiyo ikitarajiwa kuhitimishwa katika kata hizo tisa na kuanza kwa kata nyingine tatu za mji huo ambazo ni Utengule, Kitandililo na Mahongole.
Waliojitokeza kwa wingi kuajiandikisha katika mji huo ni vijana akinamama na wazee waliokuwa na vitambulisho, waliopoteza na wale ambao ilikuwa mara yao ya kwanza kujiandikisha baada ya kufikia umri wa kupiga kura.
Kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yeyote aliyefikia umri wa miaka 18 anaruhusiwa kupiga kura, hivyo ili apate haki hiyo analazimika kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura na kwa mwaka huu tume ilitoa ruksa kwa watu wanaotarajia kufikia umri wa miaka 18 siku ya kupiga kura kujiandikisha.
Msimamizi wa Uchaguzi Mji wa Makambako Vumilia Nyamoga alisema tume imevuka lengo na kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na ushirikiano waliofanya kati ya tume, serikali, viongozi wa vyama vya siasa na wale wa dini kuwatangazia watu kujitokeza kwa wingi kujiandikisha.
Alisema kata tatu za Utengulile, Kitandililo na Mahongole zinatarajia kuanza kazi ya uandikishaji leo kama ratiba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilivyoelekeza.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mwembetogwa Patrick Mhagama alisema kazi hiyo imefanikiwa kutokana na kazi waliyoifanya ya kutembelea nyumba kwa nyumba kuhamisha watu kujiandikisha. Mmoja wa wakazi wa mtaa wa Mwembetogwa, Michael Mkongwa alisema watu wengi wamejitokeza kujiandikisha kutokana na kupewa elimu ya uraia.
“Watu wameguswa na mambo yanayotokea nchini na vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi na wametambua kuwa wao ndio wenye mamlaka ya kuchagua viongozi bora,” alisema .
Mkongwa na kuongeza:
“Nitumie fursa hii kuwataka wanasiasa na viongozi walioko madarakani kama wanataka kubaki katika nafasi zao wajipima na wawe waadilifu kwani wasipofanya hivyo wananchi hawatakuwa na namna nyingine zaidi ya kuwaadhibu kwenye sunduku la kura”alisema.
Kwa upande wake Sudi Nyagawa kutoka mtaa wa Mjimwema alisema kazi ya uandikisha imeenda vizuri hasa baada ya tume kuongeza siku mbili na huku akisistiza kuwa kitam kitumbulisho alichokipata atakitumia vizuri kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment