Friday, March 20, 2015


Mr Muganyizi akiwa na wafanyakazi wa AccessBank katika moja ya maeneo ya mawakala kushoto Ismaili kati Malosha
Wateja wa AccessBank Tanzania wameendelea kuipongeza na kuishukuru AccessBank kusogeza huduma zake karibu nao kupitia mawakala wake maarufu kama AccessBank WAKALA.


Kupitia mfumo huu mpya yulioanzishwa na benki hiyo, sasa wateja wanaweza kufanya miamala mbalimbali kwa urahisi Zaidi katika maeneo walipo pasipo  kulazimika kwenda kwenye matawi ya benki. Huduma mbalimbali kama vile kuweka, kutoa fedha, kufungua akaunti na huduma zingine nyingi zimeendelea kufanyika kwa urahisi Zaidi kupitia mawakala hao.
Naye Afisa Masoko Mwandamizi wa AccessBank, Mr Jonas Muganyizi Bisheko, amewaasa wateja kuendelea  kujipatia huduma za kibenki mahala popote waonapo Bango la AccessBank WAKALA.
Kwa sasa mawakala hao wanapatikana maeneo yafuatayo; SKUVI MINI SUPERMARKET(kijitonyama Shule- 0784 800573), LACASUMBAI(Nyuma ya Tawi la AccessBank Kijitonyama- 0717 173084) na JK INTERNET CAFÉ( Mwenge Mpakani- 0713 477112)

Aidha, Mr Muganyizi amesema kuwa mawakala wengine katika maeneo mbalimbali watatangazwa    hivi karibuni

0 comments:

Post a Comment