Friday, March 20, 2015


Name:  Kinana barabara.png
Views: 0
Size:  414.5 KB


Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndugu Abdulrahman Kinana umekuwa kivutio kikubwa katika mitaa mbalimbali jijini Arusha, ambako yuko katika Ziara yake ya Kikazi kwa siku mbili.

katibu Mkuu amepata mapokezi makubwa Eneo la Baraa alikoanzia Ziara yake na Kisha kuelekea Elerai ambapo akizungumza na wagonga kokoto na kuwatatulia kero yao ya kunyanyaswa na viongozi wa Kata ambao wanataka kuua Eneo hilo kwa Mtu Binafsi anayeitwa Singh.

Pia ameshiriki uchimbaji wa mtaro wa bomba la Maji Olkaryan, Olasit Pamoja na kukagua ujenzi wa Barabara ya Sombetini- Njiro Kisha kuzungumza na Wananchi wa Sombetini na kuwataka kuchagua Viongozi ambao wana "uwezo" wa kuwaletea maendeleo.

Katibu Mkuu atembelea Soko la Kilombero lililopo Kata ya Sombetini Jimbo la Arusha na kusikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara Sokoni hapo ambapo wafanyabiashara wamelalamika kupanda kwa bei ya kodi kutoka 30,000 mpaka 200,000/=

Kinana amtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kufanya kikao na uongozi wa Soko la Kilombero tarehe 2/4/2015 kujadili suala hilo la kupanda kwa Kodi.

LAKINI pia amtaka Meya na Mkurugenzi kufanya maamuzi bila kushirikisha wananchi na kukubaliana nao ili kuhepuka kero za mara kwa mara, na kuwaagiza kuacha kukusanya kodi hiyo iliyopanda mpaka pale watakapokubaliana na uongozi wa Soko juu ya kima stahiki cha kodi.

Katibu Mkuu anaendelea na ziara yake kwa kutembelea na kufungua matawi 24 map ya ya CCM katika Kata Mbalimbali jimbo la Arusha Mjini.


Quote By security guard View Post
KUKUBALIKA KWAKE KWA DHIHIRIKA LEO ARUSHA MJINI ALIPOTEMBELEA SOKO LA KILOMBERO NA KULA CHAKULA KWA MAMA LISHE SOKONI HAPO.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu hoja mbali mbali zilizoletwa na kamati ya soko la Kilombero ikiwa pamoja na kupandishiwa kodi bila utaratibu maalum.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Arusha kwenye soko la Kilombero ambapo walisalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali wakila chakula kwa Mama Lishe wa soko la Kilombero,jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wa wananchi baada ya kuzindua shina la kikundi cha wajasiriamali Oysterbay Unga Ltd.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakinywa kahawa mara baada ya kumaliza kuwasalimu na kuzindua shina la wakereketwa wajasiriamali Oysterbay, Unga ltd, Arusha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wengine wa CCM kuelekea kwenye soko la Kilombero,jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wanananchi wakati akiwasili kwenye soko la Kilombero lililopo jijini Arusha.

Wananchi na wafanya biashara wa soko la Kilombero ,jijini Arusha wakimpa mikono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

0 comments:

Post a Comment