Monday, March 23, 2015

1
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukitembelea jengo la NHC lililoungua mwaka jana mjini Singida ambapo Shirika linajenga upya jengo jingine katika kiwanja hicho kilichoko katikati ya mji huo. Jana Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia kyando Mchechu ameanza ziara yake ya kutembelea Mikoa ili kuhimiza utendaji kazi wa viwango na kujionea utekelezaji wa miradi ya nyumba za gharama nafuu katika mikoa atakayotembelea ya Singida, Shinyanga, Tabora, Kigoma, Sumbawanga,Katavi na Mbeya. Picha na Muungano Saguya-Shinyanga
New Picture (2)
Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu ukiwa eneo la Unyankumi na kupewa maelezo ya mradi wa nyumba za gharama nafuu na Meneja wa NHC Mkoa wa Singida Bw. Ladislaus Bamanyisa ulipotembelea mradi huo kukagua ujenzi wake.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za gharama nafuu eneo la Unyankindi Singida na kukuta mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizoakiwa amejenga ukuta usilingana na viwango vilivyowekwa na NHC katika miliki zake inazojenga.
New Picture (4)
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu na ujumbe wake wakiwa na mfanyakazi aliyestaafu utumishi wake NHC Dr. Allan Kabogo (wa pili kutoka kulia) walipomkuta eneo la Misigiri Wilaya ya Iramba akiwa anajishughulisha na biashara na huduma za kitabibu. Ujumbe huo ulifurahishwa kuona mstaafu wa NHC anaishi maisha ya furaha na matumaini makubwa.

0 comments:

Post a Comment