Picha
Haina Uhusiano Wowote na Tukio HiliMTU mmoja amefariki dunia na
mwingine mmoja kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota
(Mchomoko) lililokuwa likitokea Manyovu kuelekea Kigoma Mjini na
kugongana na pikipiki katika eneo la Mlole-Sido lililopo Manispaa ya
Kigoma Ujiji mkoani humo.
Akizungumza Kigoma24hours Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, SACP Fredinandi Mtui, alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku katika eneo ambapo gari aina ya Toyota lenye namba za usajiri T616 DXR lililokuwa likiendeshwa na Pitolus Silasi (33), lilisababisha ajali hiyo.
Kamanda alimtaja marehemu kuwa ni Pantoleo Philipo (30) ambaye ni dereva wa pikipiki na alikufa papo hapo huku abiria aliyekuwa amembeba katika pikipiki yake akiwa amejeruhiwa vibaya maeneo ya kichwani na kuvunjika mkono na mguu.
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari ambapo mara baada ya ajali dereva wa gari alitokomea kusiko julikana na kwamba jitihadi za kumsaka zilifanyika na kumkamata ambapo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.
Akithibitisha kupokea miili ya marehemu na majeruhi katika Hospitali ya rufaa Maweni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Fadhili Kibaya alisema majira ya usiku alipokea mwili wa marehemu pamoja na majeruhi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Michael Madyane ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa maweni kwa matibabu.
Kibaya alisema hali ya majeruhi ni mbaya na kwamba anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mifupa na hivyo kulazimika kumpatia rufaa katika hospitali ya Bugando ambapo kuna madaktari bingwa wa upasuaji huo.
Alisema licha ya hospitali hiyo kuwa ya rufaa lakini bado inakabiliwa na changamoto ya madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ambapo jitihada za maksudi zinaendelea ili kukabiliana na changamoto hiyo.

0 comments:
Post a Comment