Posted by Williammalecela.com on Tuesday, April 28, 2015
Ali Chocky (katikati) akiwa na waimbaji wenzake, Luiza Mbutu (kulia), na Kalala Junior baada ya kutambulishwa.
Wanamuziki
wa ‘Twanga’ wakiongozwa na Kalala Junior (kushoto) wakiwa na begi
ambalo ndani yake alikuwemo mnenguaji Super Nyamwela kama moja ya staili
ya kutambulishwa.
Baadhi ya wanenguaji wa bendi hiyo wakifungua begi hilo tayari kwa utambulisho wa mnenguaji mwenzao, Super Nyamwela.
Nyamwela akionyesha manjonjo yake baada ya kutambulishwa.
Wanenguaji wa kike wa bendi hiyo wakiwajibika jukwaani.
Nyamwela akiongoza safu ya wanenguaji muda mfupi baada ya kutambulishwa.
Wanenguaji wakichapa kazi jukwaani.
ALIYEKUWA
Mkurugenzi wa Bendi ya Extra Bongo, Ali Chocky, na mnenguaji wake,
Super Nyamwela, usiku wa kuamkia Aprili 26 walitambulishwa rasmi ndani
ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, aliporejea
bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’. Choky ni ataendelea kuwa mmoja
wa waimbaji wa bendi hiyo ambapo atafanya kazi sambamba na Luiza Mbutu
na Kalala Junior. Nyamwela ataungana na wanenguaji wengine kuimarisha
safu ya wasanii wenzake
0 comments:
Post a Comment