Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za
kukutwa na viungo vya mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino).
Watu
hao wanatuhumiwa kufukua kaburi la mtu huyo na kuchukua kila kiungo cha
mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Bartazar John, aliyefariki
mwaka 1991.
Hatua
hiyo imechukuliwa na jeshi hilo zikiwa zimepita siku saba tangu watu
wengine wawili kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika kuuza viungo vya
marehemu Wilaya ya Muleba, mkoani humo.
Kamanda
wa Polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, alisema watu hao walikamatwa
Machi 27, mwaka huu, katika nyumba moja ya kulala wageni, iliyoko eneo
la Kyaka, Wilaya ya Missenyi baada ya kukutwa wakiwa na baadhi ya viungo
hivyo, ambavyo walikuwa wanakwenda kuviuza.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Laston Faustine (41), ambaye ni mkazi wa
Lukulaijo aliyekutwa na mfuko uliokuwa umehifadhi mifupa mitatu ya
binadamu na mwingine ni January Korongo (43), mkazi wa Kadengesho,
wiyani Karagwe.
Kamanda
Mwaibambe alisema baada ya kumbana, mtuhumiwa wa kwanza, Laston
aliliambia Jeshi la Polisi kuwa aliyempa viungo hivyo ni mwenzake,
January, kwa ajili ya kuviuza kwa Sh. milioni 20.
Baada
ya kuhojiwa, January alikiri kufukua kaburi la mjomba wake, aitwaye
Baltazari aliyekuwa na ulemavu wa ngozi albino pia mlemavu wa viungo,
ambaye alifariki dunia mwaka 1991 na walifukua kaburi lake mwaka 2009.
Mwaibambe
alisema baada ya kumhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na
polisi hadi nyumbani kwake, ambako alionyesha fuvu la kichwa, mifupa
mitatu ya miguu pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali, ambayo ilikuwa
imefungwa kwenye mfuko nje ya nyumba yake.
Polisi
waliomba kibali cha Mahakama Wilaya ya Karagwe kuruhusiwa kufukua
kaburi hilo ili kuhakikisha kama kweli kuna mabaki ya mwili huo, lakini
hakuna kilichopatikana.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment