Hali likuwa hivi:
Mnyika: Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima, mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njome, jambo hili ni la dharura na ilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie, majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano hamna kitu.
Makinda: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza
Mnyika: Amegoma na sauti zimekua nyingi na fujo zimeanza
Makinda: Anang'ang'aniza katibu aendelee na wabunge wa upinzani wamesimama na kutaka majibu kwanza
Katibu: Muswada wa habari
Wabunge: Kwa sauti waliosimama, wanaendelea kupiga kelele wakisema "tunataka majibu..tunataka majibu". tumechoka kuburuzwa..Makinda kwanini unailinda Serikali..Vurugu zimeanza bungeni.
Makinda:Nimesema majibu mtajibiwa baadae
Wabunge: Tunataka sasa hivi kwani Waziri Mkuu yupo
Spika Makinda: Naahirisha bunge hadi jioni.
0 comments:
Post a Comment