Baada ya mkuu wa jeshi la polisi nchini kuvipiga marufuku vyama vyote vya siasa kuhusu kuwa na makundi ya kujihami katika vyama hivyo, CHADEMA wamekaidi agizo hilo halali la polisi na wameendelea kuwatumia Red Brigedi katika chama chao!
Jambo ambalo CHADEMA hawakutarajia ni kuwa, polisi wana vyanzo vyingi vya taarifa, hivyo mmoja wa makamanda wa CHADEMA alifikisha taarifa kwa jeshi la polisi juu ya uwepo wa vifaa vya kivita ndani ya ofisi ya makao makuu na pia kuna mpango wa kusambaza vifaa hivyo kote nchini.
Zifuatazo ndio picha za vifaa hivyo na jinsi CHADEMA ilivyojipanga kuandaa waasi ikitokea imeshindwa uchaguzi mkuu! Yale yanayotokea Kongo yataletwa Tanzania kama serikali haitachukua hatua juu ya jambo hili.
Baada ya vijana wa CHADEMA kuwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi wakiwa na vifaa hivyo vya kijeshi.
Vifaa hivyo vikiwa vimekusanywa kwa pamoja na jeshi la polisi ambapo awali vilikuwa vimefichwa maeneo mbalimbali ndani ya ofisi ya CHADEMA na vingine vikiwa tayari kwa kusafirishwa kwenda mikoani.
Hapa pia tunaweza kujionea wenyewe jinsi CHADEMA walivyojipanga kuivuruga amani yetu kwani hakuna chama cha siasa kinachoweza kuwa na zana hatari za aina hii ofisini!
KWA WALE MNAODHARAU VISU KUTUMIKA KAMA SILAHA ZA KIJESHI, HEMU TAZAMENI HIVI VISU AMBAVYO NI MAALUMU KATIKA JESHI LA MARAKENI NA UTUMIKA PIA VITANI.
Pia itakumbukwa ni hivi karibuni tu kuna magaidi walikamatwa Morogoro wakiwa na vifaa vifuatavyo: silaha za sub machine guns, milipuko ya kulipulia majengo majambia, manati, bendera nyeusi, sare za jeshi nk. Hivyo kuna uwezekano mkubwa magaidi hao wakawa na uhusiano na vijana hawa wa CHADEMA. Hivyo jeshi la polisi halina budi kufanya upelelezi wa kina ili kuzuia vitendo vya kigaidi nchini.
Mnamo tarehe 24/4/2015 huko maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE TABLEI SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana na taarifa za kiintelijensia.
Watu hawa walikamatwa wakiwa na buti pair 2 za kijeshi, kofia pair 2 za kijeshi, kamba kurukia ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara), manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1, Pamoja na barua 3 za CDM za kata ya MSANGANO, SHITETE, na KAMSAMBA (W) MOMBA zenye kichwa cha habari "UTOAJI WA VIONGOZI WA RED BRIGED KATIKA KATA YENU KWA MAFUNZO YA RED BRIGED".
Barua inasomeka hivi
Husika na kichwa cha barua hapo juu chajifafanua vema.
Napenda kukujulisha kuwa kutakuwa na ziara ya kimafunzo ya RB (Red Briged) katika kata yenu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Na kwa barua hii naomba uwapokee na uwape ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.
Ni matumaini yangu kuwa utawapokea na kuwatunza pamoja na usalama wao.
Wako katibu wa chama Wilaya.
Katika mahojiano vijana hawa walikuwa wakienda kutoa mafunzo ya kijeshi katika kata tajwa na mpango wao ni kufundisha vijana 300 katika wilaya ya Momba na mpango huu ni wa mkoa na Nchi nzima chini ya Mkurugenzi wa Usalama Taifa CDM bwana LWAKATARE.
Monday, April 27, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments:
Post a Comment