Thursday, April 23, 2015

KISA NGOZI YANGU.

Hawapendi rangi yangu,
Yawaudhi ngozi yangu,
Nalilia roho yangu,
Kisa ngozi yangu.


Silali nikatulia,
Nalala naweweseka,
Nalia nahangaika,
Kisa ngozi yangu.



Mbona sishangai yao,
Hata wao wana yao,
Wamekaza macho yao,
Kisa ngozi yangu.


Salamu kwao wenzangu,
Wanipende ndugu zangu,
Wanilinde ngozi yangu,
Kisa ngozi yangu.



Tuishi sawa na ndugu,
Kama zamani udugu,
Bila chuki na vurugu,
Kisa ngozi yangu.
 
Tenzi Almasi.

0 comments:

Post a Comment