
Ni biashara ya ngono ikiwamo ya jinsia moja ,Wasichana wazungumza suluba wanazopata
Mwanamke
mmoja, mkazi wa Mabibo Mwisho, jijini Dar es Salaam, anadaiwa kuanzisha
danguro la wasichana na kuendesha biashara ya ngono ikiwamo ya jinsia
moja.Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la mama Uzuri, anadaiwa
kuwachukua wasichana hao kutoka vijijini kwa kuwadanganya kuwa anakwenda
kuwatafutia kazi mjini Inadaiwa kuwa fedha anazopata kutokana na
biashara hiyo, huzitumia kama gharama ya kuwatunza wasichana
hao.Wakizungumza Jumapili kwa nyakati tofauti, wasichana hao (majina
yanahifadhiwa), walidai kuwa mwanamke huyo aliwachukua vijijini kwao kwa
ahadi ya ajira za ndani.
Wakielezea undani wa biashara hiyo,
walisema wanaume wengi wamekuwa wakiwalazimisha kufanya mapenzi bila
kinga (kondom), kwa madai kuwa kwa kufanya hivyo kunawanyima starehe ya
tendo hilo.
Suzana (sio jina lake halisi), alisema makazi yao ni
nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo hulelewa katika mazingira mazuri, na
kati yao kuna makahaba na wasagaji.
Alisema, mwanzo walipoanza biashara hiyo walipata wakati mgumu lakini kadiri siku zinavyokwenda waliizoea.
0 comments:
Post a Comment