- Leo tena ajali Nzega imeua Mwananchi Mmoja na kujeruhi vibaya wegine 20, Akili moja ndogo sana huko Serikalini akaamini Kuwalazimisha Madereva kwenda Shule na kuwalipisha Shillingi Laki Tano ndio jawabu. Ninasema hivi 95% ya ajali za magari ni PREVENTABLE, nilipokuwa ninasoma USA nilikuwa ninaendesha 18 Wheel Trucks yaani Malori yenye Matairi 18 nilikuwa na Leseni inayoitwa "Class A" CDL Commercial License ambayo kuipata ni almost impossible unless una AKILI KUBWA kwa sababu inahitaji kusoma sana Darasani na Barabarani, halafu hata ukishatimiza masharti yote bado kuna sharti moja kubwa la mwisho nalo ni once ukiwa na hiyo Leseni unaitwa "Professional Driver" maana yake ni kwamba ukipatwa na ajali wakati wowote ule ni your full responsibility unless proven otherwise by the authorities.

- Madereva wa Mabasi na Malori makubwa ni lazima wawe na Leseni za namna hii, na ukishafikia hiyo level ya kuwa na hiyo Leseni ni lazima Kampuni inayokuajiri ijue kabla hujaingia kazini kama umepumzika Masaa 10 toka ulipoacha kuendesha last na incase Supervisor wako ana wasi wasi haupo sawa anaruhusiwa na Sheria kukupa kipimo cha Pombe au Drugs kabla ya kukuruhusu kuingia kazini kuendesha. Serikali kila mwezi inapitia kwenye Makampuni husika na usafirishaji kutoa Elimu na kuhakikisha Kampuni zipo sawa na Sheria ya barabarani na usafiri kwa ujumla, wala sio mambo makubwa sana kuyafanya kuepusha ajali za ajabu ambazo zinaua wananchi wetu bila sababu ya msingi.

- Mfano mdogo ni Kabla ya Waziri Mwakyembe kushika Wizara ya Uchukuzi, Bandari ya Dar ilikuwa inaingiza mapato ya Shilling Billioni 40 tu, likini within mwezi mmoja wa kuishika yeye Mapato yakaongezeka mpaka Billioni 150 kwa mwezi siku moja nililimuuliza miujiza aliyoifanya akasema nothing but kuamuru Wateja wote wa Bandari kulipia malipo Benki tu imetuchukua Miaka 53 ya Uhuru kwa Kiongozi mmoja wa Serikali ya CCM kufikiria wazo dogo sana kama hilo, Ukweli ni kwamba Bandari yetu inatakiwa kukusanya Billioni 300 ina maanabado kuna Billioni 150 inayopotelea mikononi mwa wajanja mpaka leo ndio maana hapa mjini matajiri karibu 90% ni walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na TRA, now my point here ni kwamba hata huko barabarani kinachotakiwa kufanyika wala sio kitu kikubwa sana kuondoa hizi ajali ila hakuna anayejali maana tutasikitika siku moja au mbili then tumerudia tulipokuwa inaitwa Insanity kurudia njia ile ile ukitegemea matokeo tofauti.

- Ninasema umefika wakati wa Serikali ya CCM kuamua kwamba enough na ajali na kusimamia sheria au kutunga Sheria mpya, inashangaza majuzi Serikali imetunga Sheria mpya kali za Cyber Crimes lakini sio Sheria kuhusu ajali barabarani WHY? Kwa sababu habari za mitandao zinawagusa Wanasiasa ila ajali haziwaguzi sana so ni sawa sawa tu, it is wrong na ni wakati muafaka wahusika wa hiyo Sekta wakajiuzulu wenyewe au wafukuzwe kazi, ingawa na sisi wananchi tunahusika sana kwa kuchagua maviongozi magoi goi kila mwaka haya ndio matokeo yake, wanakuja kwenye mazishi wanaona huzuni na vilio vyenu lakini hawawezi kwenda Bungeni kusema lolote kuhusu ajali na vifo vingi vinavyotokea kila siku na ajali halafu wakija tena kuomba kura mnawapa na kuwafurahia kwa kupewa pilau!!

- Nchi zote zilizoendelea Duniani zinakuwa na System ya kutafiti kisayansi Mwaka mzima na mwisho wa Mwaka inatoa maelezo ya chanzo cha Vifo vingi kwa Taifa kwa ule Mwaka na kuiachia Serikali itafute jawabu, sisi sijui hata kama tuna chombo kama hicho tungekuwa nacho isingewezekana tukawa na ajali zote hizi bila jawabu. Jamani enough Serikali fukuzeni wote wanaohusika na hii sekta cause wameshindwa na ni wote wahusika tuanze upya kwa kweli hii sekta ni moja ya pungufu kubwa sana la Serikali ya CCM, ni wakati muafaka wa Serikali kukubali hadharani huu upungufu na kuufanyia kazi haraka sana kama Sheria hazitoshi zitungwa haraka lakini haiwezekani tukapoteza wananchi kila siku na ajali na huku Serikali imekaa kimya sio sawa.


Le Mutuz