Rukia Fikiri(kulia) akiwa na nd
ugu zake wakiwa wamebeba maiti ya mtoto wanaodai kubadilishiwa na manesi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
Baba wa mtoto akihojiwa na mtndao huu
Rukia Fikiri anayedai kubadilishiwa mtoto huyo.
Wakiingia hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kuiludisha maiti hiyo n
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
SKENDO mpya
imeikumba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kufuatia mwanamke
mmoja, Rukia Fikiri (pichani) kudai kujifungua mtoto wa kiume kisha
baadaye kukabidhiwa mtoto wa kike akiwa amefariki dunia, Uwazi
linatiririka.Tukio hilo la kushangaza lilijiri Machi 25, mwaka huu
katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.
MSIKIE MWENYEWE
Akizungumza
na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita hospitalini hapo, Rukia alisema
alijifungua mtoto wa kiume mwenye afya njema saa 6 usiku wa Machi 24,
mwaka huu na kwamba baada ya kujifungua alionyeshwa kisha aliondolewa
leba na kupelekwa Wodi ya Wazazi 7 B.
“Lakini kutokana na uchungu wa
uzazi kule wodini nilipitiwa na usingizi. Nilipokuja kuamka, manesi
waliokuwa wakinihudumia na mtoto wangu waliniambia mtoto amefariki
dunia.“Niliumia sana, nilitoa taarifa kwa ndugu zangu akiwemo mume wangu
ambapo walifika hapa tukakabidhiwa maiti huku manesi wakisema
wameifunga kwa nguo, wakasema tukaifungulie nyumbani,” alisema Rukia,
akaongeza:
“Tulienda nyumbani kwa wakwe zangu eneo la Chamwino.
Tulipofungua maiti kwa lengo la kuiosha ili tukaisitiri, tulishangaa
kuona ni ya mtoto wa kike badala ya wa kiume.”“Haraka sana tukagundua
manesi walitubadilishia. Tulikaa kikao cha dharura cha familia,
tukakubaliana tuirudishe maiti hapa. Mimi ninamtaka mtoto wangu wa kiume
awe hai au amekufa,” alisema mwanamke huyo huku akiangua kilio kwa
uchungu.
MUME NAYE AZUNGUMZA
Mume wa Rukia, Hamidu Fikiri naye alipata fursa, akazungumza na Uwazi na kusema:
“Kitendo
walichofanya wale manesi ni cha kushangaza sana, kama nisipopewa
mwanangu tutaelewana vibaya, mimi nimeshakwenda polisi.”
Mama mzazi
wa Hamidu, Mariam Seif ambaye ni bibi wa mtoto alisema kitendo cha
mjukuu wake ‘kuibwa’ wodini kimemsikitisha na hawezi kuzika mtoto wa mtu
mwingine.“Tulipomrudisha mtoto hapa hospitalini, manesi walikuwa
wakitupiana mpira, wale wa wodi 7 B wanasema tatizo liko leba, wa leba
wanasema kinyume chake,” alisema bibi huyo.Taarifa zinasema, polisi
waliamuru mwili wa mtoto huyo uhifadhiwe hospitalini hapo huku uchunguzi
ukiendelea.
Uwazi lilipompigia simu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Mkoa wa Morogoro, Rita Lyamuya hakupatikana ofisini kwake na hata
alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa.
MASWALI MAGUMU
Ndani
ya cheti cha mzazi kulazwa na kuruhusiwa kuna maandishi ya msingi wa
uzazi yanayosomeka: Complete Abortion ‘CA’ (mimba kuharibika)
ikimaanisha ndicho kiini cha mzazi huyo kufikishwa hospitalini hapo.
Uwazi lilijiuliza kwa nini cheti hicho kiandikwe hivyo wakati mzazi anadai alijifungua salama tena leba?
Daktari
mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo), alipoulizwa na
gazeti hili kuhusu hali hiyo, alisema: “Complete Abortion ni mimba
imetoka kabla ya muda wa kujifungua. Lakini kama huyo mama aliingizwa
leba ina maana alijifungua, wasingeandika Complete Abortion, wangeandika
SB, kwamba amejifungua salama.
“Mwanamke wa CA hawezi kupelekwa
leba. Kutakuwa na tatizo katika uandishi wa hicho cheti. Kwani mtoto
mwenyewe alikuaje hata kama alifariki dunia?”Uwazi: “Mwili wa mtoto upo
kamili, ila ni marehemu tu.”
Dokta: “Sasa CA mtoto hawezi kuwa kamili. Nadhani hapo katika uandishi wa cheti pana tatizo.”
Gazeti ili linaendelea na uchunguzi.
a kudai mtoto wao.
0 comments:
Post a Comment