Posted by Williammalecela.com on Thursday, April 16, 2015
Imelda
Mtema STAA wa filamu Bongo, Wema Sepetu na Mtangazaji Penniel Mwingila
‘Penny’ ambao wote kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kuona
habari za mwenza wao huyo wa zamani akiwa na mpenziwe mpya, Zali
zinapamba moto kila siku, wameibuka na kudai hawababaishwi nazo, kwani
hivi sasa wameamua kuingia kazini kwa kufanya bonge la project.
Mtangazaji
Penniel Mwingila ‘Penny’. Akizungumza kwa niaba ya mwenzake, Penny
alisema kelele za kila siku wamezichoka na baada ya kukaa pamoja,
wameona hiki ni kipindi cha kupiga kazi badala ya kupoteza muda.
Staa
wa filamu Bongo, Wema Sepetu. “Tumeamua kuandaa filamu yetu ya pamoja
ambayo ninaamini itakuwa ni kali na ya aina yake. Tumepoteza muda mwingi
na hivi sasa tunahitaji kufanya kazi, tunachowaomba mashabiki wakae
tayari kutupokea na hatutaki tena kushabikia mambo ya Zari na Diamond
kwa sababu hayatuhusu,” alisema.
0 comments:
Post a Comment