Wimbo huo ambao utakuwa ni single ya nne kwa msanii huyo kutoka jiji la miamba Mwanza utatoka Jumatatu April 13.
‘Nitazoea’ ni wimbo wa Mapenzi ambao umetayarishwa na ma-producer watatu ambao ni Aby Daddy, Lollipop na D-Classic.
video ya ‘Nitazoea’ itaanza kufanywa wiki ijayo na Adam Juma wa Next Level.
Nyimbo za Mo Music zilizopita kabla ya huu ni ‘Basi Nenda’ ambayo
ilifanya vizuri kila kona ya nchi, na kufuatiwa na ‘Simama’ pamoja na
Almasi ambazo zilitoka kwa pamoja mwishoni mwa mwaka jana.

0 comments:
Post a Comment