Staa
wa filamu za Kibongo, Esha Buheti amesema anajipanga kumtafuta msanii
mwenzake Issa Musa ‘Cloud’ ili amuombe msamaha akiamini bila kufanya
hivyo mambo hayawezi kumnyookea.Esha alisema yeye na Cloud ni kama mtu
na kaka yake lakini kwa hali ilivyo inaonekana kama msanii mwenzake huyo
ana kinyongo naye hivyo atakwenda kumuomba radhi ili tofauti zao
ziondoke.
Staa wa filamu za
Kibongo, Esha Buheti. “Yaani nimekaa na kuona ipo haja ya mimi kumtafuta
na kumuangukia Cloud ili kama kuna kitu nilimkwaza anisamehe kwani
naona kama mambo hayaniendei vizuri,” alisema Esha huku akidai anajua
kinachomfanya Cloud ‘ammaindi’ ni kitendo cha yeye kutangaza kujitoa
Bongo Muvi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment