Thursday, April 23, 2015


"Nikiwa kama kijana mzalendo ambaye ni mwanachama na kiongozi wa CCM nasikitishwa
sana na hii tabia ya sasa ya watu hasa vijana kujitia vimbelembele kwa utashi na ushabiki wao hadi kufikia kutukana viongozi bila uoga wala aibu tena kwa majina.Hii tabia inasikitisha sana,hivi huwezi kunadi na kumwaga sera za mgombea unayempenda mpaka umkashifu na kumtukana mtu anayeonyesha nia ya kugombea nafasi hiyo?

 (Ukizingatia ni haki ya mtu) Jeuri na maadili ya kutukana mtu mzima unaitoa wapi? (Wewe unayeshabikia akitukanwa baba yako utafurahi?) Unaposema fulani mgonjwa uliwahi mpa mke wako akamshindwa? Au ww umepima afya yako? Eti fisadi.. mtaje unayemtaka ww ambaye sio fisadi watu wamjadili.Mbaya zaidi kashfa hizi zinatoka kwa Mwana ccm kwenda kwa Mwana ccm (unampa nani faida?) Kisa umfurahishe fulani au ukidhani utapewa U DC.

Simtetei mtu ila nachukizwa na tabia iliyojitokeza ya watu kujitia ujuaji na kutukana watu wazima (eti mpaka unafinyafinya pua na kuigiza kigugumizi cha Nyerere..UNAFIKI MTUPU) Kila mtu ana uhuru wa kuchagua na kupenda lakini huna uhuru wa kumsemea mwenzako uongo uhalalishe upuuzi wako.Yoyote atakayeteuliwa na Ccm ndio huyo tutakayembeba na kumshangilia Iwe 

EL,Membe,PM au yoyote kutoka ccm ni wetu tu,usifikie mahali ukaja kuona haya kwa utumwa wako na adabu yako mbaya wakati hawa Viongozi wenyewe hawana uadui wa maisha.Nimezungumza haya ni ya kwangu binafsi ingawa pia binafsi yale maandamano ya washawishi yananikera mno lakini nashauri vijana tuwe na adabu na uadilifu."

0 comments:

Post a Comment